Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (Kulia) pamoja na
Waziri wa Elimu,Ufundi,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako
wakiwasili katika ukumbi wa Bunge kushiriki kikao cha 9 cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Askari wa Bunge akiweka Siwa katika ukumbi wa Bunge kuashiria kuanza kwa
kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson
akiongoza kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji wakatiakitoa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba,2014 wakati wa kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Ufundi,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako
akiwasilisha Taarifa ya mwaka ya chuo Kikuu Cha Dodoma kwa mwaka wa
Fedha 2013/2014 katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Mhe.Dkt
Hussein Ali Mwinyi wakati wa katika kikao cha 9 cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
No comments:
Post a Comment