ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 23, 2016

BAYPORT YAKABIDHI HATI ZA VIWANJA VYA VIKURUTI

Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed (kushoto), akishuhudia bwana James Moses Lubinza akitia sahihi katika tukio la upewaji wa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani leo mchana, jijini Dar es Salaam. Lubinza alikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport. Huduma hizo za viwanja mwaka huu zinaendelea kwa kuanzishwa miradi ya Bagamoyo, Kigaamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa vikuhusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Picha kwa hisani ya Bayport Financial Services.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services Ngula Cheyo katikati akikabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti kwa mteja wao James Moses Lubinza leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.

Afisa Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akiangalia mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma wakati anatia sahihi katika makabidhiano ya kupewa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma.
Mwanasheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akipiga picha ya pamoja na mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma baada ya kumkabidhi hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani leo mchana.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imekabidhi hati za viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa baadhi ya wateja waliomaliza kulipa mikopo yao tangu walipochukua mikopo hiyo yaa viwanja mapema mwaka jana. Baadhi ya wateja waliokabidhiwa hati hizo ni pamoja na Desidery Didas Kalimwenjuma wa Temeke na James Moses Lubinza wa Kimara jijini Dar es Salaam, huku hati za wateja wengine zikiwa zimekaamilika kwa ajili ya kukabidhiwa wateja hao ambao walikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, vilivyokuwa vinauzwa na Bayport kwa kushirikiana na Kampuni ya Property International Ltd.
Akizungumza leo mchana katika makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema ni furaha yao kubwa kuanza kutoa hati ya viwanja vilivyouzwa kwa baadhi ya Watanzania walioamua kuchangamkia fursa za viwanja vyao. Alisema hatua hiyo ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati vinakuwa sehemu ya kuendeleza na kusaidia wananchi ambao kwa kupitia viwanja hivyo wanaweza kuvitumia katika fursa mbalimbali kama vile mikopo, kujenga nyumba za biashara na makazi ya kuishi wao na familia zao.

“Hii ni hatua muhimu kwetu Batyport kuona viwanja vya Vikuruti vimeanza kutoka kwa hati zao na kuona kila aliyepata kiwanja basi hatakuwa na usumbufu wowote wa kupewa hati yake, iwe kwenye mradi wa Vikuruti au maeneo mengine ya Tanzania tunayoendelea na biashara ya kuuza viwanja kwa njia ya fedha taslimu na mkopo.

“Tunawahakikishia usalama na huduma bora kabisa kutoka kwetu Bayport, tukiamini kwamba viwanja vyenye hati tunavyotoa ni maeneo mazuri na yanayoweza kujibu maswali rahisi ya Watanzania wote kuweza kumiliki ardhi kwa utaratibu rahisi na mzuri,” alisema Cheyo.
Akizungumza baada ya kupewa hati yake, Kalimwenjuma alisema anashukuru kwa kupata hati yake haraka bila usumbufu wowote, hali inayoonyesha umakini mkubwa uliokuwapo kwenye huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport. “Nashukuru kwa sababu nilikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport na leo nimepigiwa simu kwa ajili ya kukabidhiwa hati yangu huku nikiwa na furaha kubwa pamoja nja kuwapongeza mno kwa huduma bora,” Alisema.

Naye Lubinza alisema hajawahi kukutana na huduma bora za viwanja kama vya Bayport kwa sababu havina longolongo wala usumbufu wowote, jambo linaloonyesha utulivu na umakini uliozalisha kupewa hati yake haraka bila tatizo. “Ni maendeleo makubwa kwa kuwekeza fedha zangu kwa kununua viwanja vya Vikuruti nikiamini kuwa ardhi ni kitu kinachopanda thamani siku hadi siku, huku nikifurahia zaidi kwa sababu ni miongoni mwa Watanzania waliopewa hati na Bayport,” Alisema.

Maeneo mengine ya Tanzania ambayo Bayport inatoa mikopo ya viwanja ni pamoja na Bagamoyo (Kimara Ng’ombe), Kibaha (Boko Timiza), Kilwa (Msakasa), Kigamboni (Tundi Songani) na Chalinze katika maeneo ya (Kibiki na Mpera), ambayo Watanzania wote wakiwamo watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali wanaweza kupata fursa ya kukopeshwa viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati na kuidhinishwa na mamlaka zote za Serikali kupitia kwa wabia wao wa kibiashara.

Kwa viwanja vinavyoendelea kukopeshwa, wilayani Kilwa eneo la Msakasa kilomita moja ya mraba inauzwa kwa Sh 2000, Chalinze ni Sh 4500, Bagamoyo Sh 10,000, Kigamboni Sh 10,000 na Kibaha mkoani Pwani mita ya mraba itapatikana kwa Sh 9000.

No comments: