Meneja wa kampeni ya Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala (katikati) akionyesha miongozo hiyo kwa waandishi wa habari, kulia kwake ni Mratibu wa Ukaguzi na Tathmin wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Wilbard Mkama na kushoto kwake ni Mratibu Kikundi Kazi Misitu Tanzania, Cassian Sianga.
Balozi wa Kampeni ya Mama Misitu, Asha Salimu alizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa miongozo hio
Kampeni ya Mama Misitu (MMC) kwa
kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii Machi 23, 2016 imezindua miongozo
miwili rahisi ya usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja na uvunaji katika
misitu ya hifadhi ya jamii.
Miongozo hiyo ambayo imetokana na
miongozo ya Kiingereza ambayo awali ilichapishwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii mwaka 2013, inalenga kurahisisha kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya
uhifadhi na uvunaji wa rasilimali za misitu kuanzia ngazi za taifa hadi kwa
wananchi wenyewe.
Meneja wa kampeni hiyo Gwamaka Mwakyanjala anasema iliwalazimu kuiweka
miiongozo hiyo katika lugha rahisi ya Kiswahili ili kuwezesha wananchi kuelewa
na kuchukua hatua. “Miongozo ya awali ilikuwa katika lugha ya kingereza na
hivyo kukwaza zoezi la uelimishaji kwa wananchi, tunaamini kwa kutumia miongozi
hii iliyo kwenye lugha ya Kiswahili ujumbe utafika kwa walengwa na kampeni yetu
itafanikiwa pia” anasema Gwamaka.
Uzindui huo ambao ulifanywa chini ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) ulihudhuria na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa
habari, viongozi mbalimbali kutoka taasisi za serikali na mashirika binafsi.
Mkurugenzi wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF),
Ben Mfungo Sulus akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa miongozo hiyo
Wadau wa Misitu wakifuatilia mkutano huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Waandishi wa Habari za Mazingira
Tanzania (JET), John Chikomo akizungumza juu ya umuhimu wa wanahabari katika
kutoa elimu ya mazingira
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment