Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo
Jeddah, Saudi Arabia, Bw. Suleiman Saleh amekutana na kufanya mazungumzo
na Bw. Saleh Said Bakhatab, Mmiliki wa SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS
ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa mifugo nchini Saudi Arabia. Bw.
Saleh alimkaribisha Bw. Bakhatab ofisi kwake Jeddah na kupata maelezo ya
kina kutoka kwa mgeni wake kuhusiana na utayari wake wa kununua na
kusafirisha kwa mifugo mbali mbali kiwemo ngombe na kondoo na mbuzi kwa
ajili ya soko la Saudi Arabia. Bw. Bakhatab alibainisha kwamba kwa
miaka 25 amekuwa akinunua kondoo, mbuzi na ngombe kutoka Sudan,
Ethiopia, Somalia, Australia, Romania na Uruguay na utafiti wake
umeonyesha kwamba Tanzania ina mifugo yenye ladha nzuri kutokana na aina
ya malisho bora. Kwa mantiki hiyo Bw. Bakhatab alimuomba Konseli Mkuu
kumuandalia miadi na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wenye dhamana ya sekta hiyo ili kukamilisha azma yake hiyo.
Aidha Bw. Bakhatab alimweleza Bw. Saleh kwama kuna mambo ya msingi ambayo katika kufanikisha biashara hiyo ni vyema yakaandaliwa ili biashara ifanyike kisasa na kwa ufanisi mkubwa. Mambo hayo ni pamoja na kuandaliwa utaratibu endelevu wa kupatikana kwa mifugo hiyo kulingana na mahitaji ya soko la Saudi Arabia, Pili, kuandaa mazingira elimishi kwa wafanyakzai wa bandari na viwanja vya ndege ili wawe na ufahamu wa kina kuhudumia mifugo inayosafirishwa ambapo alionyesha utayari wake kusaidia katika kuleta video za mafunzo hayo. Tatu, ni kuandaliwa eneo mahususi la Karantini kwa mujibu wa taratibu za kiafya za kimataifa ambapo mifugo inahifadhiwa na kupata huduma ya uchunguzi sahihi kabla ya kusafirishwa. Mwisho, Bw. Khatab alipendekeza mkutano baina yake na viongozi wa Wizara husika nchini Tanzania ili kuweka mikakati ya haraka ya kufanyika kwa biashara hiyo.
Kwa upande wake Bw. Suleiman Saleh alimhakikishia Bw. Bakhatab kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.Rais John Pombe Joseph Magufuli imeanza kazi kasi ya aina yake kwa kujenga mazingira rafiki na yenye ufanisi wa hali ya juu na kumuahidi kwamba atawasiliana na viongozi wa Wizara ya Kilimo na Mifugo ili wampokee atakaposafri kutembelea Tanzania hivi karibuni.

Pichani 1. Bw. Suleiman Saleh, Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jeddah,Saudi Arabia, akimkaribisha ofisini kwake Bw. Saleh Saeed Bakhatab, Mmiliki wa Kampuni ya SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS ya Saudi Arabia.
Pichani 2: Bw. Suleiman Saleh akiendelea na mazungumzo na Bw.Bakhatab.
No comments:
Post a Comment