Na Talib Ussi, Zanzibar
CHAMA cha wananchi CUF kimewapongeza wanachama na wale waliowaita wazalendo wa nchi yao ya Zanzibar kwa kukubali ushauri wa chama hicho wa kususia uchaguzi wa marejeo kiliodai ni Batili.
Kauli ya chama hicho imetolewa na naibu Katibu Mkuu Nassor Ahmed Mazurui alipozungumza na waandishi wa habari leo huko ofisini kwake Vuga Visiwani hapa.
Alisema kukataa huko kwenda kupiga kura wameidhihirishia Dunia kwanjia ya amani na ya ustarabu kuuwa chaguo lao ni Maalim Seif sharif Hamad kuiongoza Zanzibar.
“Kwa mara nyengine tena Wazanzibar wameyathibitisha maamuzi yao ya Kidemokrasia waliyoyafanya kupitia uchaguzi huru na wa haki wa 25 octoba mwaka jana”, alisema Mazurui.
Alisema kutokana na hilo hawatambui uchaguzi wa marejeo wala hawatashirikiana wala kuitambua Serikali itakayoundwa kutokana na kile walichokiita matokeo batili.
“Chama chetu sisi kilishaeleza mapema msimamo wetu kwa hiyo hili la kuatoa mchango wowote kwa uchaguzi huu haramu halipo” alisema Mazurui.
Kupitia nafasi hiyo mazurui alivipongeza vyombo vya habari vya nje na ndani kwa kile alichokisema kuonesha hali halisi ilivyokuwa na jinsi gani wanzibar walivyoikataa CCM na watawala waliobaka demokrasia.
“Wazanzibar wameandika historia nyengine mbele ya macho ya ulimwengu na kwa mara nyengine Wazanzibar wameshindaa” alieleza Mazurui.
Alisema chama kinajua kwamba wazanzibar wanahamu ya kujua ni hatua gani zinafuata katika kusimamia maamuzi yao ya kidemokrasia waliyoyafanya 25 October mwaka huu.
“Nina waambia wananchi kwamba, Chama chao hakijayumba na wala musiwe na ghofu na kinafuatilia haki yao kwa njia za amani na za kidemokrasi na kitakuwa kiinatoa maelezo kwa kila kinachoendelea” alieleza Mazurui.
Chama cha wananchi CUF hakikushiriki uchaguzi wa marejeo kwa madai kwamba uchaguzi huo ni batili.
No comments:
Post a Comment