Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO),
imetangaza kuwako na ongezeko la Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar
es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, baada
ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza kufanya majaribio ya uzalishaji wa Maji
.
Akiongea na waandishi wa habari kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO,
Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo la Maji watu
wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na pia kumekuwepo na ongezeko la uvujaji
wa Maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam, hasa katika maeneo ambayo
yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji na baadhi ya
maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo (Low pressure)
“Kufuatia ongezeko hili la Maji watu wengi wameanza kupata huduma
ya Majisafi, na uvujaji wa Maji umeongezeka katika maeneo ambayo aidha yalikuwa
na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji au maeneo ambayo
yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo” Alisema Bi. Lyaro.
Aidha, ametoa wito kwa wateja na wananchi wote kutoa taarifa za
uvujaji huo wa Maji pindi wanapobaini kuwapo na uvujaji wa Maji katika makazi
yao na maeneo mbalimbali ya jiji kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga
simu namba 022194800 au 0800110064 (Bure).
“Namba hizi ziko wazi saa 24 kwa siku na mteja hatakatwa gharama
yoyote akipiga simu hizi. Hivyo tunaomba wateja wetu waisaidie Dawasco
kupunguza upotevu wa maji kwa kutupa taarifa za mivujo na kupasuka kwa mabomba”
alisema bi Lyaro.
Kutokana na ongezeko hilo la Maji maeneo yaliyoanza kupata Maji
baada ya majaribio ya mtambo huo kuwa ni Tandale,Manzese
makunimula,Mwananyamala,Kinondoni mkwajuni, baadhi ya maeneo ya
vingunguti,changombe,ubungo-mabibo na city centre.
Pia, DAWASCO imetumia nafasi hiyo kuwakumbusha wateja wote kulipia
huduma ya Maji kwa wakati kwani watu wengi kwa sasa wameanza kupata huduma ya
Majisafi na salama kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa Maji katika mtambo
wa Maji wa Ruvu chini, hivyo hawana budi kuyalipia ili kuepuka usumbufu wa
kusitishiwa huduma ya Maji.
Kuongezeka kwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na Mji
wa Bagamoyo kumetokana na
kukamilika upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini ulioanza mwaka 2011 hivyo kuongezeka
kiasi cha uzalishaji wa Maji kutoka wastani wa lita milioni 182 hadi lita 270
kwa sasa.
No comments:
Post a Comment