ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 24, 2016

KONSELI MKUU WA UBALOZI MDOGO WA TANZANIA JEDDAH,SAUDI ARABIA, ATEMBELEA ENEO LA KUHIFADHIA MIFUGO LA SALEH BAKHATAB MJINI MECCA

Kufuatia ziara ya Bw. Saleh Saeed Bakhatab Jumanne Machi 22, 2016, katika Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia, Konseli Mkuu Bw. Suleiman Saleh, nae Jumatano Machi 23, 2016, alimtembelea mfanya biashara huyo mwenye makazi yake katika mji wa Mecca ili kuona aina ya mifugo ambayo anaiagizia kutoka nchi za nje.

Wakati wa ziara hiyo Bw. Saleh alipokelewa katika mji wa Mecca na Bw. Bakhatab ambaye kwa kiasi kikubwa alifarijika na uharaka wa ziara hiyo ya ufuatiliaji siku moja tu baada ya yeye kutembelea Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia. Bw. Bakhatab ambaye yumo katika maandalizi ya kutembelea Tanzania alimkaguza Konseli Mkuu katika eneo analopokelea mifugo ya aina mbali mbali ikiwemo ya ngamia, ngombe, kondoo na mbuzi . Bw. Bakhatab alimueleza Bw. Saleh aina mbali mbali ya mifugo hiyo na namna anavyoihifadhi na kuipatie lishe stahili ili kukidhi viwango wa soko la Saudi Arabia. Aidha, katika ziara hiyo, Bw. Bakhatab alimuhakikishia Bw. Saleh kwamba anaamini kwamba Tanzania itakuwa moja ya chanzo kikuu cha kampuni yake kununua mifugo ya aina mbali mbali na hivyo kusaidia juhudi za Serikali za kuinua uchumi wake .

Bw. Saleh Saeed Bakhatab anaemiliki kampuni ya SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS amejizatiti katika kufanya biashara ya mifugo na Tanzania, amejipanga kusafirisha mifugo hiyo kwa ndege maalum kutoka Tanzania hadi Djibouti ambapo baadae itapakiwa katika meli hadi Jeddah, Saudi Arabia akiijumuisha na mifugo kutoka nchi za Sudan na Somalia.

 Pichani ni Bw. Suleiman Saleh Konseli Mkuu wa Ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah,Saudi Arabia, akiwa na Bw. Saleh Saeed Bakhatab wakiwa katika eneo lake la kuhifadhia mifugo anayoiagizia kutoka nje katika mji wa Mecca, Saudi Arabia. 











No comments: