Thursday, March 3, 2016

Mama yake Halima Mdee alia na serikali ya Magufuli


Mama mzazi wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mama Theresia Mdee ameilalamikia Serikali ya Awamu Ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kutokana na yanayomsibu mwanae.
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi kupekuwa nyumba ya Halima Mdee, ambaye wiki hizi mbili zilikuwa chungu kwake baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi na kulazwa rumande.
Mama huyo alieleza kuwa kinachofanywa na serikali dhidi ya mwanae ni uonevu wa dhahiri na kumnyima haki.
“Hii serikali kwakweli tunaona kwamba haitutendei haki. Hayo yote wanayomfanyia huyu mtoto hakuyafanya. Wanamuweka ndani bila sababu, wanakuja kumsachi hakuna kitu… ni kiasi cha kumuumiza tu na kumkandamiza ili asiweze kufanya kitu,” alisema.
Hata hivyo, Mama huyo alitahadhalisha kwamba vitendo hivyo vinavyofanywa dhidi ya mwanae huenda vikawa chanzo cha kumkuza zaidi, “Sasa wajue kwamba wanamtia moshi”.
Mdee alishikiliwa na polisi kufuatia vurugu zilizoibuka katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kutangaza kuahirisha uchaguzi. Uliokuwa umepangwa kufanyika siku hiyo (Jumamosi, Februari 27).

3 comments:

Anonymous said...

Badili ya kukaa na kuitupia lawama serikali,anapaswa amweleze mwanae aachane na siasa za ki magumashi.Chadema waliposhinda uchaguzi wa Madigan na umeya wa Kinondoni, ilala Halina Mdee na kundi lake walijitokeza adharani wakijitapa kuipiga serikali changa la macho kwa kutumia kalamu zenye camera. Yanayomkuta sasa hivi ni matokeo ya mdomo wake..

Anonymous said...

Nchi bila ya watu wake kutii na kuheshimu sheria ni chanzo cha matatizo yote. Kuwa mbunge wa upizani sio sababu ya kutotii sheria za nchi na kuchochea vurugu hata kama kuna uthibitisho wa haki fulani kutotendeka kuna taratibu za kisheria ambazo mtu anaweza kupeleka malalamiko yake na kusikilizwa kwa njia za amani baada ya kutumia njia za vurugu. Nadhani kuna watu wanataka kutafuta umaarufu kwa kutumia njia haramu,njia za vurugu. Mchezaji hawezi kwenda kumpiga referee au kukataa kutoka nje ya uwanja kwa sababu mwamuzi katoa red card kimakosa, la kuna taratibu zake za kufuata ili haki ipatikane badala ya vurugu.

Anonymous said...

Halima anechaguliws kutetea haki za wananchi wa mtanzania. Vurugu mnayoongelea hapo ni ipi? Watanzania amkeno. Mmezoea kuburuzwa tuu. Hata Mandela alipelekwa gerezani kabla ya kupata ukombozi. Go halima go!