ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 31, 2016

Uchunguzi usafirishaji wa Tumbili wakamilika

By Daniel Mjema, Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz

Moshi. Kikosi kazi maalumu cha kuchunguza makosa ya kihalifu kimekamilisha uchunguzi wa tuhuma za usafirishaji Tumbili 61 zinazowakabili raia wawili wa Uholanzi na Watanzania wawili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alilithibitishia gazeti hili jana kukamilika kwa uchunguzi huo na kusema jalada limepelekwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.

Kauli ya Mutafungwa imekuja wakati kuna uvumi uliozagaa kuwa watuhumiwa hao wataachiwa huru wakati wowote kuanzia jana bila kufunguliwa mashtaka.

Kamanda Mutafungwa alisema kuwa wao kama chombo cha uchunguzi, wametimiza wajibu wao na mwenye uamuzi wa kushtaki au kutoshtaki ni Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) baada ya kupitia ushahidi.

Hata hivyo, alisema kuwa watuhumiwa hao wanne bado wanashikiliwa na polisi wakisubiri maelekezo ya kisheria ya DPP, hivyo siyo sahihi watu kuvumisha kuwa wameachiwa bila masharti.

Watuhumiwa hao ni Mkurugenzi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, Utalii wa Picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika. Watuhumiwa wengine ni raia hao wa Uholanzi ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik Vardanyian (52) na Eduard Alik Vardanyian (44).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alipoulizwa juzi kuhusu uvumi wa kutoshtakiwa kwa watuhumiwa, alisema yeye ametimiza wajibu wake.

5 comments:

Anonymous said...

Nuksi ya MCC

Anonymous said...

Anonymous Anonymous said...
Ndugu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya maliasili,Tunaiomba sana kamati yako itufanyie uchunguzi wa waziri wa maliasili na utalii Bwana Magembe,kwa kufanya maamuzi ambayo hata hakufanyia uchunguzi wa kusimamisha biashara ya viumbe hai bila kufuata taratibu,eti kwa kisingizio cha tumbili wanaotoroshwa.sasa imethibitika kuwa yeye kapigiwa simu na mfanya biashara mmoja wa wa kirusi hapa dar es salaam (ambaye ana leseni ya nyara hapa Tanzania) kuwa kuna tumbili wanatoroshwa na hawana vibali bila kufanya uchunguzi ukweli huyu mrusi baada ya kukosa soko la kuuza hao ngedere kwa waholanzi ndio walioshinda tenda Armenia (waliokamtwa) ya kuuza hao ngedere kaamua kuwafanyia fitina kwa kueneza habari za uongo kuwa hawa jamaa hawana vibali wakati wanakila kitu,je waziri anawezaje kumsikiliza mtu tena mfanya biashara binafsi bila kufanya uchunguzi wa kuwashilikisha wataalamu wa wizara yake??? je hawa ndiyo mawaziri wa magufuli wanaokulupuka tu bila kufanya uchunguzi na kujichukulia sheria za kibabe siyo kuwatumikia wananchi walioplipia vibali na bila taarifa anaamua anavyotaka.hii serikali ya wapi isiyofuata sheria mtu anaamua tu

Anonymous said...

NI JAMBO LA KUSIKITISHA SANA TENA SANA,HUYU WAZIRI MALIASILI HAFAI NILISHACHANGIA KWENYE BLOGU MBALI MBALI NA KUSEMA KUWA HUYU WAZIRI KAKURUPUKA WAPO WALIONIPONDA KWA KUWA WATU HAWAJUI NATURE YA HII BIASHARA,WATU WA WATU WAMEWEKWA NDANI,NDEGE IMEZUIWA BILA KUBEBA MZIGO,WAMEDHALILISHWA NA KIBAYA ZAIDI MTUHUMIWA MMOJA MKEWE ALIPOPATA HIYO HABARI KUWA MMEWE AMEKAMATWA TANZANIA NA AMEWEKWA NDANI ALIPATA MSHITUKO LEO AMEKUFA,NI AIBU KWA NCHI KAMA HII KUWA NA MAWAZIRI MIZIGO WASIOHESHIMU HATA WATAALAMU WAO,INAKUWAJE WAZIRI MZIMA UNAPIGIWA SIMU NA MFANYABIASHARA WEWE BILA KUCHUNGUZA HATA KUWASHIRIKISHA WATAALAMU WALIOCHINI YAKO UNAKULUPUKA KUTANGAZA KWA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI KWA NCHI NA KUWAINGIZA WATU HASARA LEO MMEONA UKWELI MTAENDA LIPA HASARA KWA MAMILIONI,HII NI AWAMU YA TANO YA KUKULUPUKA KUTAKA SIFA ZA MAJIPU YA BILA KUWA NA UHAKIKA.

Anonymous said...

Biashara ya Nyara hai ( TDL) INASIMAMIWA NA SHERI YA BUNGE YA WANYAMA PORI NO. 5 YA MWAKA 2009...PAMOJA NA KANUNI ZAKE .
INFANYIKA KUPITIA MADARAJA ( CLASSES ) 13,
MOJA YA MADARAJA HAYO NI NO. 13 AMBAYO NI PRIMATES ( NGEDERE,TUMBILI NA NYANI) NA WAMEORODHESHWA AINA ZAKE NA IDADI.....KWA MWAKA TUNARUHUSIWA KUSAFIRISHA PRIMTAES 5000..
PIA PRIMATES HAO NI MOJA YA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO WAKUBWA...
BIASHARA HII HUFANYIKA KITAALAMU KUZINGATIA SHERIA ZA TA NZANIA NA ZILE ZA KIMATAIFA ( CITES ), KWANI BIASHARA HII NI YA KIMATAIFA HIVYO HAINA USIRI WA AINA YEYOTE. IPO WAZI....HUFANYWA NA WATU WALIOOMBA LESENI WIZARANI KILA MWAKA KUFUATIA TANGAZO LA WIZARA KAMA SHERIA INAVYOTAKA..NA UKAGUZI HUFANYIKA KUHAKIKISHA WAOMBAJI WANA UWEZO WA KUWATUNZA.
KABLA YA KUKAMATWA WANYAMA HUSIKA LAZIMA WALIPIWE IDARANI TENA KWA THAMANI YA US DOLLAR YA SIKU HIYO, PIA LAZIMA WAPIMWE NA VETERINAY DOCTOR WA SERIKALI NA KUPEWA HEALTH CERTIFICATE HUSIKA..
PIA UASAFIRISHAJI WAKE LAZIMA UZINGATIE SHERIA ZA USAFIRI WA ANGA KIMATAIFA ( IATA- LAR ) BIASHARA HII HUINGIZA SERIKALINI FEDHA ZA KIGENI AMBAZO NI MUHIMU SANA...
mATUMIZI YA WANYAMA HOTE HUSIKA HUFANYIKA KWA KUZINGATIA MATUMIZI ENDELEVU ( SUSTAINABLE UTILIZATION )..ILI KUHAKIKISHA IDADAI YAO HAIPUNGUA NCHINI....VIGEZO VYA KITAALAMU HUTUMIKA.MAMBO HAYA YOTE YAPO WIZARANI KWA KILA MTU ....TATIZO LA SISI WATANZANIA HATUPENDI KUJUA UKWELI , TUNAPENDA MANENO YA BARABARANI YASIYO NA UKWELI.REJEA KWENYE SAKATA LA TWIGA,,,,NANI ALIFUNGWA???
NI VIZURI MKAWA MNAULIZA ILI MUELEWESHWE BADALA YA KUHISI MNAJUA.. NA KUULIZA SI UJINGA...JE MKIJA ELEWA KUWA TATIZO HILI LA NGEDERE LIMEPOTOSHWA NA WATU AMBAO SI WATANZANIA KWA SABABU ZAO ZA KIBIASHARA BINAFSI MTAJISIKIAJE..???
NCHI YETU NI TAJIRI, ILA SISI WENYEWE TUNASHINDWA KUNUFAIKA IPASAVYO KWA SABABU NI RAHISI KUDANGANYWA NA WAGENI....TUNAFIKIRI WAZUNGU WOTE WANAJUA KILA KITU, KWA HIYO KILA ANACHOKUAMBIA MZUNGU TUNAONA NI KWELI..TUSIONEE WATU KWA FAIDA BINAFSI...NDIYO MAANA TUNASISITIZA HUYU WAZIRI WA MALIASILI AMEKULUPUKA TU KWENYE HII SAKATA YA UTOROSHWAJI HAO NGEDERE HABARI HIZI SI ZA KWELI

Anonymous said...

Ni vema baadhi ya Mawaziri kutenda mambo kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi ili wasiumize wananchi bila sababu za msingi...Ebu fikiria, wananchi wamepewa leseni halali kusafirisha nje ngedere ( class 13 ) halafu unasitisha biashara kwa sababu tu kuna mtu ( mzungu - mrusi ) amekupigia simu akakudanganya kuwa kuna tumbili wanasafirshwa nje kimagendo....Kama kuna kosa kwanini asiadhibiwe mhusika anayehusika tu ??
Ndugu zangu Watanzania, huyu Mrusi aitwaye David Z...ni mtu mwenye dharau sna kwa nchi hii,anauhusiana mkubwa na baadhi ya watu Serikalini kwa ushirikianao wa vigogo wa Kiasia wanaomiliki mahoteli makubwa nchini,,,, shida yake kubwa ni kuwa anataka biashara ya nyara hai ambayo kisheria haruhusiwi aifanye yeye tu hapa Tanzania kwa kushirikina na hao vigogo wa Kiasia...
Mrusi huyo hat Uhamiaji eti wanamwogopa,,,yaani ni ajabu sana....
Ameivuruga sana biashara yetu huko nje hasa huko kwao urusi ..
Serikali tunaomba mtuondolee mtu huyu nchini kwetu ili kuinusuru biashara yetu adhimu..
Mungu Ibariki Tanzania.