Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi wilayani Hai (UVCCM),Arnold Swai amepinga ya kurejea ndani ya chama
hicho kwa mwanadiplomasia na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Juma Mwapachu.
Balozi Mwapachu, juzi alitangaza kurejea
CCM kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.
Akizungumza na wanahabari jana mkoani
hapa,Swai alisema kuwa chama hakipaswi kumpokea mwanasiasa huyo kwa madai kuwa
ni msaliti huku akienda mbele zaidi na kutaka waliompokea wachukuliwe hatua za
kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za chama.
"Ni lazima tujiulize, hivi
mwanadiplomasia huyo angekuwa tayari kurejea CCM kama mgombea urais wa UKAWA,
Edward Lowassa angeshinda urais?" alihoji na kuongeza:
"Hatuwezi kumpokea msaliti
kama huyu, wakati chama kilipokuwa kwenye mapambano aliondoka tena kwa
kejeli, leo chama chetu kimesimama imara chini ya mwenyekiti wetu Rais mstaafu
Jakaya Kikwete, ndio anarudi na wimbo uleule kwamba chama kimemlea,
haikubaliki."
Alisema wakati wa kampeni kuelekea
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,baadhi ya makada maarufu wa CCM walikisaliti chama
huku wakitoa kauli za kejeli na kusababisha mpasuko ndani ya chama ambao
majeraha yake hayajapona.
Mwenyekiti huyo alieleza kukerwa na
kauli ya Balozi Mwapachu kwamba chama ndo kimemlea na kwamba hayo si
maradhi ya kumuua mtu bali yanatibika, lakini dhambi ya usaliti haitibiki
"Nguvu kubwa iliyotumiwa na CCM
kuwanadi wagombea wake ilisababishwa na wasaliti kama hawa,nawaomba viongozi wa
ngazi za juu kutofumbia macho jambo hili kwani ni hatari kwa ustawi wa chama
chetu." Alisema
Balozi Mwapachu alirejea CCM juzi na
kupokelwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Athuman
Mareenda, ambaye alimkabidhi tena kadi ya uanachama wa chama hicho.
1 comment:
Tugange yajayo. Huyu mzee ni makini sana katika mambo ya sheria na hasa sheria zinazohuzu biashara za hali ya juu. Bado ana mchuzi mwingi wa kuipa nchi yetu inayohitaji zaidi biashara kubwa imara zitakazotoa AJIRA ZA MAANA hasa kwa vijana, biashara zitakazokuwa na uwezo wa kutoa huduma ndani ya nchi na hasa zaidi kutoa huduma nje ya nchi ili uuzwaji wa huduma na bidhaa nje ya nchi ulete mapato makubwa zaidi nchini. Tumieni huo ujuzi wake wa kipekee. Tugange yajayo.
Post a Comment