Advertisements

Wednesday, April 27, 2016

BIMA YA AFYA YA AAR YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI HOSPITALINI AMANA

Ikiwa ni wiki amabayo ya Malaria Duniani, Mataifa mbaliombali Duniani hutumia nafasi hii kufanya shughuli mbali mbali katika kuadhimisha wiki na siku ya Malaria duniani.

Kampuni ya Bima ya AAR imetembelea Hospitali ya Amana iliyoko Ilala Dar es salaam na kutoa msaada wa vyandarau kwa wamama wajawazito katika kutimiza lengo la kupunguza uenezi wa gonjwa la Malaria.

Akiongea na wandishi Habari Hospitalini hapo, Afisa Mahusiano wa kampuni ya bima ya AAR, Bibi Amisa Juma alisesema, “Tukiwa kama wadau wa Afya Tanzania, ni jukum letu katika jamii kuonyesha mfano wa kupambana na maradhi mbalimbali ikiwemo hili Malaria.

Hii imakua ni utamaduni kwa kampuni ya Bima ya AAR kuadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kushirikiani na Jamii katika shughuli mbali ikiwemo kuchangia kutoa elimu juu ya kujikinga na tiba pamoja na kuchangia matibabu kwa jamii tofauti ya Tanzania. Almalizia Bibi Amisa.

Wafanyakazi wa AAR walitembelea hodi ya kina na mama wajawazito na watoto na kutoa msaada huo.

No comments: