Serikali imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kutekeleza kwa umakini miradi ya kusambaza umeme katika vijiji ambavyo bado havijapata huduma hiyo.
Akijibu swali la mbunge wa Bukene, Sulemani Zedi aliyehoji hatua ambazo Wakala wa Umeme Vijijini (REA) imechukua dhidi ya mkandarasi (CHICCO) ambaye ameshindwa kukamilisha utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme vijijini awamu ya pili huko Mbutu na Mwangoye, naibu waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dk Medard Kalemani amejibu kwa kusema:
“Awali mkandarasi CHICCO kutoka China alishinda zabuni ya usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa wa Tabora ingawa alianza kutekeleza miradi hiyo kwa kusuasua.”
Naibu huyo ameeleza kuwa baada ya REA kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo ya kumuandikia barua ya kutoridhishwa na kazi, mkandariasi huyo alianza kutekeleza miradi hiyo kwa kasi.
Amesema kazi ya kupeleka umeme vijiji vya Mambali, Mbutu na Mwangoye iliendelea na kwamba imekamilika kwa asilimia 100 kwani hadi sasa wateja 49 wameunganishwa.
Amesema kazi ya kujenga njia ya umeme imekamilika, taratibu za ufungaji wa transfoma zinaendelea na umeme unatarajiwa kuwashwa mara baada ya zoezi hilo kukamilika.
No comments:
Post a Comment