Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Iringa imetulipia mbali kesi mbili za kupinga matokeo ya udiwani zilizofunguliwa na makada wa CCM baada ya kukubaliana na hoja kuwa kesi hizo zilifunguliwa nje ya muda unaotakiwa kisheria.
Kesi ya kwanza iliyotupwa ni Namba 50 ya mwaka 2015 iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea udiwani wa Kata ya Mkwawa, Thobias Kikula dhidi ya Oscar Kafuka, msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa Serikali.
Kesi nyingine ni Namba 48 ya mwaka 2015 iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea udiwani wa Kata ya Kitwiru, Paulo Lunyunga dhidi ya Baraka Kimata, msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa Serikali.
Akisoma kwa pamoja hukumu za kesi hizo kwa maelezo kuwa mazingira yake yanafanana, Hakimu Mfadhiwi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya alisema baada ya kupitia pingamizi na kusikiliza pande zote mbili, amekubaliana na upande wa utetezi kuwa kesi zilifunguliwa nje ya mda uliopangwa kisheria.

No comments:
Post a Comment