ANGALIA LIVE NEWS
Friday, April 1, 2016
Makonda awatangazia waendesha bodaboda neema
By Vicky Kimaro, Mwananchi Digital
Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda leo na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.
Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya Sh25,000 kwa wiki kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.
Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.
Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la kuingia katikati ya jiji kutokana na agizo la aliyekua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.
Waendesha bodaboda hao wamemhakikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima la ulinzi iwapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Makonda ameanza kujichanganya.Huwezi kupigana vita ya ujambazi na mauaji jiji Dar wakati huohuo una facilitate logistics za uhalifu huo.Ili kwenda sawa inabidi Makonda atambue tofauti ya nafasi za uongozi za kichama na kiutawala.Ki msingi alipaswa kuwa ameshazipitia hizo sheria na kujadiliana na idara husika kabla hajaongea na wananchi.
tatizo la makonda ndio mfano mzuri wa viongozi wetu wa Tanzania ! tunapenda kufanya kazi au kutoa maamuzi kwa mwendo wa Zima Moto ! hakuna mipango endelevu ya kuendelea mpaka miaka 30 ijayo au na zaidi ! mipango namaamuzi ya viongozi wetu ni yamuda mfupi sana ! mipango yao yote inakoma kipindi cha uchaguzi mwingine ! kwa mwendo huo safari ni ndefu sana !
Vijana ndio kundi kubwa katika jamii ya Tanzania kuwa karibu nao ndio kuwa Tanzania, Makonda si mpumbavu kaliona hilo.
Kuna namna nyingi ya ku-connect na society lakini linapokujja swala la usalama wa raia anapaswa kuwa mwangalifu.
Vijana hao hao ndio wanaotoa hizo pikipiki kwa matukio ya wizi yanayojiri jijini kila siku, kuhakiki silaha sawa ukigeuka unatoa pikipiki, sasa huo ujambazi na mauaji yataisha jijini. Kabla hatujasifia Makonda kwa kutaka kusikia tufikirie mbelena tutokako!
Huyu huyu ndie yule Paul Makonda aliyeagizwa kumsema Lowasa kwenye mtandao na baada ya miezi akapewa ukuu wa wilaya!!
Post a Comment