Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka.
Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji ,
Maeneo mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment