
Kamanda wa Polisi Kanda ya
Dar es Salaam Kamishina Simon Siro, akionyesha marobota 10 ya vitenge pamoja na katoni 17 za Pampasi zilizokamatwa zikiwa katika
gari yenye namba za usajili T 490 CQB katika
eneo la Gezaulole
jijini Dar es Salaam jana. Baada ya askari polisi kupata taarifa kwa raia wema kuwa eneo hilo kuna watu wanasafirisha mali hiyo ambayo haijalipiwa ushuru. (Picha na Francis Dande)

Kamanda wa
Polisi Kanda ya Dar es Salaam Kamishina Simon Siro akionyesha pikipiki
zilizokamatwa katika matukio mbalimbali ya kiuharifu zikiwa katika kituo kikuu
cha Polisi, ambapo amewataka wahusika kufika kituoni na kuchukua pikipiki zao kabla hazijapigwa
mnada.
1 comment:
Asante kamanda hapo ni mkoa wa Dar ambapo Mkuu wa mkoa PM ametoa mpya ya kuwapatia vijana pikipiki kwa malipo ya tsh. kadhaa!! Ni jambo la kushangaza kuwa tunapotaka kudhibiti vitendo vya wizi unaoshamiri siku hizi kwa kutumia pikipiki Mkuu huyu anasahau yote na kuwa ameomba uhakiki wa silaha! yoote ukitizama kwa akili pevu hatutakuwa na mafanikio hayo!! Kma hizo hela anazo nyingi sana au ameunganisha na benki kutoa hiyo hela ya kununulia pikipiki ni kwa nini basi usianze na hali ya madawati jijini na vyoo vya shule kwa manufaa ya wanafunzi walioongezeka kwa kasi kubwa!1
Tusifanye kazi kwa kutaka kuandikwa magazetini na mitandao bila kutafakari! Yote heri tu hebu kwanza chukueni idadi ya hizo pikipiki zilizoko barabarani na je zimesajiliwa zote na kodi inalipwa.
Post a Comment