ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 6, 2016

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME WAZINDUA RASMI DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO NA KITUO CHA HUDUMA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo, mchana huu. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja la kimataifa la Rusumo, mchana huu. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 6, 2016 amezindua daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo.  Zoezi hili la uzinduzi  limefanyika kwa pamoja kwa kuwahusisha  Rais Mhe. Dkt. Magufuli wa Tanzania na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, pia tukio hili limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani ni kiungo muhimu katika Ukanda wa Kati(Central Corridor), mtandao huu wa barabara unaunganisha barabara kuu ya Dar es Salaam -  Chalinze – Morogoro – Dodoma – Singida – Nzega – Tinde – Isaka – Lusahanga na Rusumo kupitia Kibingo Nakayonza hadi Kigali Nchini Rwanda. Mtandao huu utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli aliwahimiza Wananchi wa Nchi zote mbili kutumia fursa ya uwepo wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani Rusumo kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Jumuiya yetu Afrika Mashariki kwa ujumla. 
Aidha Mhe. Rais amewaasa Wananchi kulinda miundombinu kwani kuna baadhi ya wananchi wanadiriki kuiba alama za barabarani, vyuma vya madaraja na kuharibu taa za barabarani kwa baadhi ya miji, ameagiza vyombo vya usalama kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria kwa wale watakaodiriki kufanya uharibifu huo.

Aidha licha ya mradi huo kurahisha usafairishaji wa bidhaa na watu Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa alieleza faida kadhaa za mradi huo zikiwemo; kuwa ni kiungo muhimu cha kuiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Kikanda kama vile  SADC na COMESA, kurahisisha mawasiliano ya kijamii baina ya watu wa Tanzania na Rwanda, pamoja na kuimarisha uhusiano na kukuza biashara kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda na Nchi nyingine za Maziwa Makuu.

Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA. 
Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka.
 Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
 Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi  wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo

No comments: