Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi (Mb), akitoa maagizo kadhaa wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo; Prof. Wilbard Kombe na kulia kwake ni Mwenyekiti mstaafu, John Lubuva.
Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji; Prof. Wilbard Kombe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji; Bwn.John Lubuva akitoa taarifa fupi ya bodi hiyo, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
WAZIRI wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) ametangaza rasmi mwisho wa
kutumia Makampuni ya nje katika kazi za kuandaa Master plan. Mhe. Lukuvi aliyasema hayo wakati akizindua rasmi bodi
ya wataalam wa Mipango Miji Wizarani hapo.
Lukuvi amesema
nchini kuna wataalam wengi na wenye elimu ya kutosha kwa ajili ya kufanya kazi
ya kuandaa Master plan, lakini
kumekuwa na taratibu za kutafuta wataalam hao kutoka nchi za nje. Alisema; “
Ninaagiza kuwa sasa ni mwisho wa kuajiri makampuni ya nje, kazi za master plan zisimamiwe na bodi hii kwa
kutumia makampuni ya humu humu nchini”.
Ameendelea kusema
kuwa’ “ Sasa Bodi ya Wataalam wa Mipango Miji itapaswa kuhusika kikamilifu
katika zoezi la Upangaji, upimaji na umilikishwaji wa ardhi kwa kushirikiana na
sekta binafsi na kuhakikisha kuwa suala la uwazi katika upangaji miji
linazingatiwa”.
Vile vile alisema kuwa
bodi itapaswa kuhakikisha Wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika kulipia
gharama kadhaa kwa huduma wanazopatiwa na bodi. Mhe. Lukuvi alisema kuwa bodi
hiyo haitaitwa tena bodi ya Mipango Miji, bali itajulikana kama bodi ya Mipango
Miji na Vijiji.
Kwa upande wake
Mwenyekiti mpya wa bodi; Prof. Wilbard Kombe alimuomba Lukuvi kuzitaka
Halmashauri kushiriki vyema katika kutoa elimu kwa umma kwa kuwa na utayari wa
kutoa taarifa zinazopaswa kuwasilishwa kwa Wananchi kwa wakati ili waweze
kuelewa vyema kuhusu mipango inayohusu maeneo yao.
No comments:
Post a Comment