ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 6, 2016

WATU WANNE WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA KIFUSI

Kamanda  wa Polisi  Mkoa  wa Kinondoni, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Christopher Fuime akiwasili katika eneo Kawe Ukwamani ambapo nyumba moja iliangukiwa na kifusi na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi watano, tukio hilo limetokea leo alfajiri jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Wananchi wakiwa wamebeba mwili wa mmoja wa watu waliofariki kwa kuangukiwa na kifusi eneoa Ukwamani Kawe jijini Dar es Salaam, leo.
 Wafanyakazi wa Uokoaji wakiwa wamebeba mwili wa mmoja waliofariki katika ajali ya kuangukiwa na kifusi leo.
Wananchi wakishiriki kuokoa miili ya watu waliofukiwa na kifusi katika eneo la Ukwamani Kawe jijini Dar es Salaam  leo.
Zoezi la uokoaji likiendelea.
Watu wakiwa wamekisanyika katika eneo la tukio kusaidia zoezi la uokoaji.
Utafutaji wa miili iliyofukiwa na kifusi ukiendelea.
Wananchi wakishirikiana na wafanyakazi wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kutafuta watu waliofukiwa na kifusi.
 Kikosi cha uokoaji kikishiriki kuopoa miili iliyoangukiwa na kifusi.
Kamanda  wa Polisi  Mkoa  wa Kinondoni, Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Christopher Fuime akitoka katika kusaiia kazi ya uokoaji wa watu wanne waliofariki kwa kufukiwa na kifusi eneo la  Kawe Ukwamani jijini Dar es Salaam.

No comments: