Ziara ya Rais Magufuli Rwanda, imeleta neema baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame, kumgawia ng'ombe watano rais wa Tanzania kama ishara ya upendo na Ushirikiano. Hii inaleta hali na Muamko mpya baina ya Tanzania na Rwanda ulokuwa umefifia kiasi cha Rais wa Rwanda kumwambia rais wa Tanzania aliyemaliza Muda wake Jakaya Kikwete kwamba "angemhit"
Siku chache baada ya Rais John Magufuli kuanza kuongoza Tanzania, harufu ya uadui kati ya Tanznaia na Rwanda ilipotea ghafla na badala yake, harufu nzuri ya ubani wa urafiki mkubwa kati ya nchi hiyo ulianza kusikika. Wakati huu pia, Rais Magufuli alivaa viatu vya Dk. Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kagame alianza kuonesha kumkubali sana Rais Magufuli kwa uongozi wake. Wawili hao walikutana na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza Machi 2 mwaka huu Ikulu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Baada ya kurudi Rwanda, Rais Kagame aliwaambia wananchi wake wazi kuwa atatumia mtindo wa Rais Magufuli katika kubana matumizi nchini kwake.
Siku chache baadae, Ikulu ya Tanzania ilitangaza taarifa ya ziara ya kwanza ya Rais Magufuli ya kikazi nchini Rwanda, ambayo ni safari yake ya kwanza ya nje ya nchi.
Wiki, Rais Magufuli alikuwa nchini Rwanda ambapo alipewa heshima ya urafiki uliotukuka na mwenyeji wake aliyemkabidhi ng’ombe wenye afya.
Akiongea na BBC, mmoja wa viongozi wa Rwanda alieleza kuwa katika utamaduni wa nchi hiyo, ni heshima kubwa kumpa rafiki yako ng’ombe. “Unakuwa urafiki uliotukuka, urafiki wa ng’ombe,” alisema kiongozi huyo.
Baadae, Rai Kagame alimfanyika hafla kubwa mgeni wake aliyeambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli.
Kwa bahati nzuri, wake za marais hao wanaweza pia kuanzisha urafiki mkubwa kutokana na mila na tamaduni za kiafrika, kwa kuwa majina yao yanafanana kwa matamshi. Ni Janeth Magufuli na Jeannette Kagame. Wanaweza kuitana ‘wa jina’ au ‘somo’.
Ni Janeth Kagame na Janeth Magufuli. Ikulu hizi mbili (Ikulu ya Kigali na Ikulu ya Dar es Salaam) kwa sasa wanaweza kuwa na ujirani kama wa nyumba kwa nyumba.
Urafiki huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hizo mbili. Bila shaka tutaona ushirikiano mkubwa wa kiuchumi kwani juzi Marais hao walizindua daraja la Rusumo, linalounganisha Tanzania na Rwanda.
1 comment:
Safi sana smart magufuli.
Post a Comment