Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea juhudi zilizofanywa na serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jana alhamis New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika pamoja na mengin kuwahamasisha viongozi wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti hali ambayo imechangia sana katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. pamoja naye ni Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji, Bw. Wolft Blitzer wa CNN.Mwanzilishi wa Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais Mstaafu, Kikwete tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili ugonjwa wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni ya Sumitomo Chemical ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z Arusha Tanzania.Sehemu ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza na kudhibiti ugonjwa wa malaria
Na Mwandishi Maalum, New York
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, anaimani kubwa kwamba ushirikiano uliopo baina ya serikali mbalimbali barani Afrika, mashirika ya kimataifa, makampuni binafsi na kila mtu katika nafasi yake, hapana shaka ugonjwa wa malaria unaweza kumalizwa kabisa.
Mhe. Kikwete ameonyesha matumaini hayo jana( alhamisi) wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jitihada za kuutokomeza ugonjwa wa malaria ( Malaria No More) zilizoanzishwa na Bw. Ray Chambers akishirikiana na Bw. Peter Chernin.
Katika hafla hiyo na ambayo mshereheshaji alikuwa Bw. Wolf Blitzer mtangazaji maarufu wa Televisheni ya Kimataifa ya CNN kupitia kipindi chake cha situation Room, Rais mstaafu alitunukiwa tuzo ijulikanayo kama White House Summit Awards ikiwa ni kutambua uongozi wake, kujitoa kwake na kubwa zaidi kusimamia uanzishwaji wa muungano wa viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria ( ALMA) muungano ambao hadi sasa una viongozi 49.
Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Sumitomo Chemical.
Akijibu swali la nini anadhani kumechangia katika kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria. Rais mstaafu amesema, zipo sababu kadhaa, lakini kubwa ni utashi wa kisiasa wa kusimamia na kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Akawaeleza wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa makapuni na mashirika mbalimbali yanayochongia juhudi za kuukabili ugonjwa wa malaria. Kwamba, Upatikanaji na usambazani wa dawa sahihi za kutibu ugonjwa wa malaria, utengenezaji, usambazaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu na unyunyiziaji wa dawa za kuuwa mazalia ya mbu ni mambo ya msingi ambayo yamechangia katika kupunguza vifi vya watoto chini ya miaka mitano.
“mchanganyiko wa mambo hayo matatu umesaidia sana kupunguza idadi ya watoto wanaofariki kwa malaria, lakini pia matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu ambapo zaidi ya vyandarua milioni 24.2 vimesambazwa, kumechangia wanafunzi kuendelea na masomo yao bila kukatishwa mara kwa mara sababu ya malaria, halikadhalia nguvu kazi imeimarika”. akasisitiza Rais Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza kwamba ugonjwa wa malaria unatakiwa kutokomezwa Barani Afrika kwa sababu unapoteza maisha ya watu wengi, bajeti kubwa katika huduma ya afya inatumika katika kutibu ugonjwa wa malaria, lakini uchumi unaathirika kutoka na nguvu kazi kuugua mara kwa mara.
Akasisitiza “ Malaria inaweza kutokomezwa. Zanzibar wameweza kutokemeza malaria, mkienda Zanzibar kutembea msiwe na wasi wasi kupata malaria”. akasema na kushangiliwa tena na wageni.
kwa upande wake, Mwanzilishi wa Malaria No More Bw. Ray Chamber, pamoja na kuelezea historia fupi ya Malaria no more ilikoanzia na ilipofika na nini mipango ya baadaye. Amemuelezea Rais Mstaafu Kikwete kama kiongozi ambaye siyo tu amekuwa mstari wa mbele katika kuukabili ugonjwa wa malaria bali pia amekuwa kiungo muhimu sana katika mapambano hayo.
“Wakati nimeanzisha juhudi hizi, nikawa natafuta mahali pakuwa na center moja na hasa kwa kuzingatia kwamba Afrika kuna nchi 43 ambazo zinatatizo kubwa la malaria, nilikuwa Benin na Mke wangu tukawa tunajadili pa kuanzia. Nikampigia simu Rais Kikwete na kumweleza nini nilichokuwa nataka kufanya. Akanijibu haya na tufanye. Sijawahi kuwa na rafiki kama Rais Kikwete na kwa ushirikiano wake tumefika hapa” akasema Bw. Chambers na kushangiliwa.
Akabinisha kwa kusema. “Kikwete amekuwa kiongozi wa kwanza kufanya kazi nami , kushirikiano wake alionipa, ushirikiano na wabia mbalimbali mkiwamo nyingi hapa katika ukumbi huu, Marais wa Marekani, Banki ya Dunia, Global Fund, Bill and Melinda Gates Foundation, tumeweza kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa asilimia 71 na tumeokoa maisha ya watu wengi.
Bw Ray Chambers ambaye pia ni mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria, anasema katika miaka kumi ya uhai wa Malaria no More lengo na mikakati waliyonayo sasa ni kutokomeza kabisa malaria ifikapo 2040.
Kwa upande wake, Mwanzilishi mwenza na Mwenyekiti wa Malaria no More Bw. Peter Chernin, amesema, katika kuonyesha ni namna gani Rais Mstaafu Kikwete amekuwa mstari wa mbele dhidi ya ugonjwa wa malaria, alianzisha na Mama Salma kampeni ya “zinduka Malaria haikubaliki” kwa lengo la kuwahamasisha wananchi na kutoa elimu dhidi ya malaria juhudi ambazo zinazaa matunda.
Akaongeza kwamba,utashi wa kisiasa upo, utayari upo, sayansi ipo, nyenzo zipo, kinachotakiwa ni fedha tu. Na kwa sababu hiyo akatoa wito kwa wadau wote wenye mapenzi mema kuchangia chochote walichonacho ili juhudi za kuokoa maisha ya watu wenzi zaidi wakiwamo watoto iendelee ikiwa ni pamoja na kuitokomeza malaria katika uso wa dunia.
Naye mwakilishi wa Kampuni ya Sumitomo Chemical, Bw. Ray Nishimoto pamoja na kuelezea kazi kubwa iliyofanywa na kampuni ya A-Z katika kutengeneza vyandarua vyenye viatilifu amesema bila juhudi na ushirikiano wa karibu aliouonyesha Rais Jakaya Kikwete kiwanda hicho kisingejengwa Arusha- Tanzania.
Akasema licha ya kutoa mchango mkubwa katika kuudhibiti ugonjwa wa malaria Kiwanda cha A-Z kimetoa ajira kwa watu 8,000 asilimia kubwa wakiwa ni wanawake na kwamba Sumitomo Chemical itaendelea na jitihada hizo.
Mhe Rais Mstaafu akiwa na Bw. Ray Chambers na Mkewe Bi. Patti Chambers muda mfupi kabla ya hafla ya kuanza.Mhe Kikwete akiwa na Bw Blitzer mtangazaji maarufu wa CNN kupitia kipindi chake cha Situation
Room
Mhe Kikwete akiwa na ujumbe wake kutoka kushoto ni Bw. Togolan Mavula, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Professa Mohamed Janabi
Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More
na Burudani pia ilikuwapo
1 comment:
Mhe JK anapeperusha bendera vyema. Asante sana.
Post a Comment