ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 26, 2016

WAKUU WA WILAYA KILOLO NA IRINGA WATULIZA HASIRA ZA WANAKIJIJI WA ILOMBILORE NA ILORE

Wananchi wa vijiji Ilambilore na Ilore wakimsikiliza mkuu wa wilaya
Mfugaji selemani akiamrishwa kulipa fidia na mkuu wa wilaya
Mgogoro ulikuwa unaashiria kuvunja amani kati ya vijiji viwili Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa) leo ulitulizwa na wakuu wilaya ya Kilolo Mh Selemani Mzee na, Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela walipofika kwenye eneo la tukio na kukutana na wananchi wa vijiji vyote viwili ambao walikuwa na hasira sana kila mmoja akidai mwenzie kaingilia eneo la mwenzake. Katika mgogoro huo eneo la kijiji cha kitongoji cha Igominyi kwenye gazeti la serikali kinaonyesha kipo Kijiji cha Ilore (Kilolo) lakini kwenye ramani ya mpaka wa wilaya kinaonyesha kipo Ilambilore (Iringa). wakuu hao waliahaidi ndani ya siku 30 wataleta jibu.

Mkuu wa wilaya ya Kilolo laipiga marufuku wananchi kujichukulia madaraka na kuanza kufyeka msitu. Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Kasesela aliagiza wafugaji wasivushe kabisa mifugo yao kwenda upande wa wenzao. Pia ni wakati mufaka wafuigaji wakaacha kuwa wachungaji bali wafugaji hii iwe ni pamoja na kubadili aina ya mifugo.

Mfugaji maarufu aitwaye Selemani alilaumiwa kwa mifugo yake kuvuka na kula mashamba ya watu. Mkuu wa wilaya ya Iringa alimuamuru Mfugaji huyo kulipa kiasi cha shilingi 90,000/ na debe 2 za mahindi. Pia kufanya tathmini ya shamba la mkulima mwingine ili nalo lilipwe fidia. kiako kiliisha saa 10 jioni.

No comments: