Wauguzi wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiendelea na kazi za mikono.
Mmiliki wa Blog ya Kajunason akimsaidia kusuka kikapu mmoja ya wazee anayelelewa katika kituo hicho.
Moja ya nyumba wanayoishi wazee hao.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliotembelea Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi wakifanya mahojiano ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili ambapo wazee hao walisema jambo kubwa linalowaumiza kicha ni upatikanaji wa matibabu katika zahanati yao jambo linalowafanya wengine kuishi na maradhi kwa muda mrefu.
Waaandishi wakiendelea kufanya mahojiano na Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi.
Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza, Michael Bundala akifanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo katika mahojiano hayo alielezea kuwa kuna changamoto nyingi za kuishi na wazee hawa kama kiongozi kwa vile wazee wamekuwa wakorofi mno na kuona siwatendei haki katika maamuzi ambayo nimekuwa nikiyatoa ikiwemo katika ugawaji wa vyakula.
-Na Cathbert Kajuna -
Mwanza.
Wazee wanaoishi katika kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaiomba Serikali kuwapatia huduma za afya katika Zahanati ya kituo chao.
Wazee hao wanaeleza kwamba changamoto hizo katika ziara ya waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliounganishwa pamoja na kuratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) na Marie Stopes Tanzania.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazee hao wanasema katika zahanati hiyo hakuna dawa na wanapoumwa wanalazimika kununua dawa.
No comments:
Post a Comment