
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Aggrey Mwanri (kushoto), wakati alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Bw. Suleiman Kumchaya.

Muonekano wa kichwa kipya cha Treni kabla ya kuanza safari katika stesheni ya Tabora. Uwepo wa hivyo vipya unatarajiwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa abiria na mizigo katika reli ya kati.
“Meneja hakikisha uzio huu unasogezwa na TANROADS wanaanza ujenzi wa barabara mara moja, Hatuwezi kuchelewesha maendeleo ya wanannchi kwa sababu ya mivutano isiyo na tija”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ameagiza nyumba tatu zinazomilikwa na Kampuni Miliki ya Rasilimali ya Reli (RAHCO) kubomolewa mara moja ili kupisha ujenzi huo na kuwaagiza RAHCO kufatilia malipo yaliyolipwa na TANROADS.
Katika Hatua nyingine amezitaka taasisi 29 zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha zinatumia huduma zinazotolewa na taasisi hizo ili kukuza uchumi ndani ya taasisi hizo.
“Naagiza taasisi zote 29 zilizo chini ya Wizara ziunganishiwe huduma ya simu ya TTCL, na zote zipeleke magari TEMESA ili kuinua uchumi ndani ya Wizarara na hivyo kunufaika na fursa ya kuwa ndani ya wizara moja”,amesisitiza Waziri Mbarawa.
Prof. Mbarawa amezitaka taasisi zilizo chini ya wizara yake kutambua fursa ya kuwa ndani ya wizara moja na hivyo kuitumia ili kunufaika kibiashara na kiutaalamu.
Aidha ametoa onyo kwa wananchi kuepuka vitendo vya hujuma dhidi ya miundombinu ya mawasiliano hususani nyaya za mkongo wa taifa ambazo licha ya nyaya hizo kutokuwa na thamani ya shaba wala dhahabu pia ni hatari kwa usalama kwani zinaweza kuhatarisha maisha.
Waziri Prof. Mbarawa amehitimisha ziara yake ya siku saba katika mikoa ya kanda ya Magharibi na kuwataka viongozi wa Serikali na taasisi zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa pamoja ili kufungua mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Tabora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikagua
kifaa maalum cha kupimia mafuta kilichofungwa kwenye kichwa kipya cha ya
Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mkoani Tabora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa , akielekea
kukagua nyumba za zitakazovunjwa kupisha upanuzi wa barabara
Tabora-Itigi, Mkoani Tabora.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment