Monday, May 9, 2016

CFAO MOTORS GROUP YANG’ARISHA BONGO CARNIVAL 2016 KWA MAGARI YA KISASA

Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Bi. Attu Mynah (kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kushoto) kwenye banda la kampuni ya CFAO Motors Group mara baada ya kuwasili katika tamasha la Bongo Carnival 2016 lililofanyika kwenye viwanja vya The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisamiana na Ofisa Mauzo Mwandamizi wa Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari ya Volkswagen, Julius Guni (aliyeipa mgongo kamera). Kulia ni Ofisa Mauzo wa Alliance Autos, Edwick Mwamba.

Kampuni ya CFAO Motors Group ambayo ndiyo wauzaji waliodhibitishwa wa magari ya Volkswagen na Mercedes Benz nchini wameshiriki katika Tamasha la Bongo Carnival 2016 ambapo bidhaa zao zimeonekana kuwa kuvutiwa na watu mbalimbali walioshiriki katika tamasha hilo.

Akizungumza na MO BLOG, Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Bi. Attu Mynah amesema walishiriki katika tamasha hilo ambalo linakujumuisha watoto mbalimbali ili kufurahi nao pamoja lakini pia kuonyesha bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo.
Alisema sehemu nyingi ambazo wamekuwa wakishiriki kumekuwa hakuna watoto lakini kupitia Bongo Carnival 2016 wamepata nafasi ya kuungana na watoto ambao wanakuwa wameambatana na wazazi wao ili kufurahi kwa pamoja lakini pia wazazi kuangalia magari yanayofaa kwa familia ambayo wanaweza kununua kutoka CFAO Motors Group yakiwa bado hayajatumika kabisa.

“Sehemu nyingi watoto wanakuwa hawapati muda wa kufurahi wao wenyewe lakini Bongo Carnival 2016 ambayo ni mara ya kwanza kufanyika imekuwa tofauti watoto wanapata nafasi ya kufurahi wenyewe lakini pia tumeleta magari ambayo ni mazuri kwa familia kwa hiyo wanaofika kwenye tukio wanapata nafasi ya kuangalia magari,” alisema Bi. Mynah.

Alisema CFAO Motors Group wamekuwa wakipinga ujangili wa wanyama kama Tembo na katika tamasha hilo kulikuwa na wanyama ili kuwapa elimu watoto kuhusu wanyama pori lakini pia kuwaeleza faida ya kutunza wanyama hao hivyo kwao ni vyema kuwapo sehemu kama hiyo ambayo inafanya jambo ambalo wao kama kampuni wanaliunga mkono ili kumaliza vitendo vya ujangili kwa wanyama pori.
Pia alisema katika tamasha hilo walipeleka magari aina ya 2016 VW Amarok, 2016 VW Caravelle, 2015 VW Tiguan, 2016 VW Toureg na 2016 Mercedes Benz ambapo gari ya VW Caravelle ilionekana kuvutiwa na watu wengi zaidi kutokana na muonekano wake lakini pia watembeleaji kupata nafasi ya kupiga picha “selfie” wakiwa ndani ya gari hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na Ofisa Mauzo wa Alliance Autos, Edwick Mwamba alipowasili katika banda la kampuni ya CFAO Motors Group katika tamasha la Bongo Carnival 2016 lilifanyika katika viwanja vya The Green, Oysterbay jijini Dar.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Bi. Attu Mynah akimuonyesha moja ya gari la kisasa (halipo pichani) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipotembelea banda la kampuni ya CFAO Motors Group kwenye tamasha hilo.
Ofisa Mauzo Mwandamizi wa Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari ya Volkswagen, Julius Guni akimunyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda jinsi siti za gari aina ya Volkswagen Caravelle zinavyoweza kujisogeza kwa teknolojia ya hali ya juu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitazama na kupata maeleo ya gari aina ya VW Passat alipotembelea banda la kampuni ya CFAO Motors Group katika tamasha la Bongo Carnival 2016 lililofanyika katika viwanja vya The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa gari aina ya Volkswagen Tiguan katika viwanja vya The Green, Oysterbay lilipofanyika tamasha la Bongo Carnival 2016.
Muonekano wa ubavuni wa gari aina ya Volkswagen Caravelle ambayo ni nzuri kwa familia ya watu wengi.
Wateja waliohudhuria tamasha la Bongo Carnival wakiendelea kumiminika viwanjani hapo kutazama gari hiyo aina ya Volkswagen Caravelle ambayo wengi walivutiwa nayo.
Aliyewahi kuwa Mrembo wa taji la Afrika Mashariki 2012, Jocelyne Maro akipiga 'selfie' na familia yake ndani ya gari aina olkswagen Caravelle ambapo kampuni ya CFAO Motors Group walitoa nafasi hiyo kwa watu waliotembelea banda lao katika tamasha la Bongo Carnival 2016.
Familia zikiendelea kupiga 'selfie' ndani ya gari hilo aina Volkswagen Caravelle.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisoma maelezo ya muundo wa gari na mifumo ya uendeshaji wa gari aina ya Mercedes Benz GLE 350 D alipotembelea tamasha la Bongo Carnival.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akitoka kutamaza gari aina ya Mercedes Benz GLE 350 D akiwa ameongozana na Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Bi. Attu Mynah alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye tamasha la Bongo Carnival 2016.
Mmoja wa washiriki wa tamasha la Bongo Carnival 2016 akiwa ndani ya gari aina Mercedes Benz GLE 350 D.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Bi. Attu Mynah (kulia) akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika katika banda la kampuni hiyo.
Baadhi ya familia zilipata nafasi ya kujaza fomu maalum na kuendesha magari hayo ili kuthibisha ubora wake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifurahi jambo na watoto waliofika kwenye tamasha la Bongo Carnival 2016 na wazazi wao.

No comments: