Mhandisi Cyprian Luhemeja. |
Akiongea
na waandishi wa habari hivi Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian
Luhemeja ameeleza kuwa kwenye awamu hii ya zoezi la uunganishaji wateja wapya
shirika litagharamia gharama zote za maunganisho ambazo ni gharama za
uunganishaji, mabomba na vifaa vya uunganishaji ambapo mteja atawajibika kurudisha
gharama hizo za maunganisho kidogo kidogo kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12
baada ya kupata huduma ya Maji.
“Dawasco
itamuunganishia huduma ya maji na kugharamia gharama zote uunganishaji ila
mteja atawajibika kurudisha ile gharama kidogokidogo kila mwezi kwa kipindi cha
miezi 12 baada ya kupata huduma ya Maji hii itasaidia hata wale ambao kipato
chao ni cha chini kuweza kuunganishiwa huduma ya Maji” alisema Luhemeja.
Pia
Mhandisi Cyprian Luhemeja ameleeza kuwa zoezi hili la uunganishia wateja wapya ni
la kipindi cha miezi miwili tu cha Mei na Juni 2016 hivyo wananchi wote watumie
fursa hii kwa kufika katika ofisi za Dawasco za kanda ili kupata huduma hiyo.
“Zoezi
hili la kugharamia gharama za
uunganishaji huduma ya maji kwa wateja ni kwa kipindi maalum cha miezi miwili
tu ambacho ni Mei na Juni hivyo wananchi watumie fursa hii kujitokeza iliwaweze
kuunganishiwa na katika kipindi chote cha zoezi Ofisi za Dawasco zitakuwa wazi
kuanzia jumatatu hadi jumapili” alisema Luhemeja.
Hata
hivyo Dawasco imeeleza kuwa wananchi pamoja wateja wake wameweza kuwasiliana na
kituo cha huduma kwa wateja kupitia
namba 022-2194800 au 0800110064 (bure) ili waweze kupata huduma na maelezo
zaidi kuhusiana na zoezi hilo la uunganishaji huduma ya Maji.
Mapema
mwaka huu serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Wizara ya
Maji, Mh Mhandisi Gerson iliagiza
Shirika la Dawasco kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya Majisafi
kutoka 156,000 waliopo sasa kufikia wateja 400,000 (laki nne) ili kwenda
sambamba na ongezeko la watu pamoja na mahitaji makubwa ya Maji yanayohitajika
katika jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment