ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 10, 2016

KAMISHNA MSAIDIZI KITENGO CHA HAKI ZA MTOTO AFUNGUA NYUMBA ZA KUNDI LA WATOTO

Kaimu Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za kundi la watoto wanaoelekea ujanani katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.
Jengo jipya lililojengwa kwa ufadhili wa Emirates National Bank of Dubai (ENBD) kwa ajili ya watoto wanaoelekea ujanani katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akimuonesha Kaimu Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo maeneo mbalimbali ya jengo hilo katika ramani.
Moja ya muonekano wa chumba katika jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo hilo.
Baadhi ya walimu na walezi wa watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center wakifuatilia shughuli mbalimbali katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akiteta jambo na Kaimu Kamishna kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akimkaribisha Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Agnes Urassa katika Hafla hiyo.

Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.
Kaimu Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa nyumba kwa ajili ya watoto wanaoelekea ujanani wa kituo cha kulelea watoto cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.
Mwakilishi wa Benki ya ENBD ambao wamefadhili mradi wa ujenzi wa nyumba hiyo,Fatma Rahman akizungumza katika hafla hiyo.
Mratibu wa miradi katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center,Jafary Salum akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo.
Wawakilishi wa Benki ya ENBD ,Rhea Fernandes na Fatma Rahman wakikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap.
Wawakilishi wa Benki ya ENBD ,Rhea Fernandes na Fatma Rahman wakionesha zawadi waliyotoa kwa watoto waishio katika kituo hicho.
Kikundi cha Sarakasi kinachundwa na watoto kikionesha umahiri katika mchezo huo.
Kaimu Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo akionesha umahiri wake katika kucheza Kwaito.
Wawakilishi wa Benki ya ENBD ,Rhea Fernandes na Fatma Rahman wakiondosha vitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: