ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 17, 2016

DKT KIGWANGALLA AWATAKA WANAFUNZI KUPENDA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba yake katika mahafali hayo huku akitoa msisitizo juu ya wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi kwa ukuaji wa uchumi.
Mku wa shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Sister Evetha Kilamba akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi pamoja na wageni wengine waalikwa katika mahafali hayo ya 19 ya kidato cha sita.


Wanafunzi Nchini hususani wale wa wa kike wameshahuriwa kujikita zaidia katika kupenda masomo ya Sayansi kwa bidii zote ili kuifanya Tanzania kufikia kwa haraka malengo yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Hii ni pamoja na Ukuaji wa viwanda vya ndani ambavyo vingi vitategemea ujuzi wa Sayansi na teknolojia.

Rai hiyo ametolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 19 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekodari ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Shule hiyo ambayo ni ya Wasichana watupu, jumla ya wanafunzi 136 wanaomaliza kidato cha sita walitunukiwa vyeti vyao vya kumaliza shule.

Dk. Kigwangalla amewapongeza wanafunzi hao 136 ambapo kati yao wanafunzi 80, ni wa mchepuo wa Sayansi ambapo amewataka kuto kata tamaa na baadala yake waongeze juhudi hadi elimu ya juu Zaidi ya ngazi ya Chuo huku pia akiwataka wanafunzi wengine hapa nchini kujikita katika masomo hayo ya Sayansi katika zama za sasa ambayo Tanzania inaelekea katika mapinduzi ya viwanda na uchumi wa Kati.

“Nina Imani na nyie. Najua hamta niangusha na mutafaulu vizuri. Nawapongeza wanafunzi wote wanaohitimu leo hii. Ni imani yangu kuwa nyote mtafaulu vizuri sana katika mitihani yenu ya kidato cha Sita kwa kupata daraja la kwanza (Division I) na wachache sana daraja la pili (Division II). Sina mashaka, najua mtailetea shule yenu (Mazinde Juu) heshima kubwa ndani na nje ya nchi” alibainisha Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hutuba maalum ya maafali hayo.

Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, katika hali ya sasa ya soko la ajira kuwa gumu, aliwataka wanafunzi hao kuzingatia kipindi hiki kifupi cha kuwa nyumbani na baadae kusubiria masomo ya elimu ya juu ya ngazi ya Chuo, kuwa watakutana na vizingiti mbalimbali hivyo amewataka kuzingatia uadilifu walioupata shuleni hapo.

“Ndugu zangu wahitimu, ni kweli kwamba nchi yenu ina changamoto ya ajira. Wasomi ni wengi lakini kazi hakuna. Kwenu ninyi tayari mna sifa kwani mnaonekana mna tabia nzuri. Pia matumaini ya kufanya vizuri kwenye mtihani wenu wa taifa. Cha maana endeleeni kuwa waadilifu na chuoni mkasome bidii. Serikali inahangaika na kazi zitaendelea kupatikana tu.

Aidha, Dk. Kigwangalla alipongeza uongozi wa shule na bodi inayosimamia shule pamoja na wazazi kwa kuwezesha shule hiyo kuifikisha hapo ilipo ikiwemo katika mafanikio ya kielimu kwa wanafunzi wanaopitia shule tokea ilipoanzishwa kwake.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Sister Evetha Kilamba ameipongeza Serikali kwa ushirikiano wanaotoa kwa Shule mbalimbali hapa Nchini ikiwemo shule hiyo ambapo pia alimpongeza Mgeni rasmi Dk. Kigwangalla kwa kuwezesha kuongeza hamasa kwa shule hiyo ikiwemo harambee iliyoendeshwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Walimu shuleni hapo.

Naye Mbunge wa Lishoto, Mh. Shabani Omari Shekilindi alitoa wito kwa wanafunzi hao kuzingatia maadili mema nje ya shule na kujiandaa na elimu ya Chuo huku akiwataka kuzingatia suala la elimu katika maisha yao.
Baadhi ya wanafunzi wa waliohitimu kidato cha Sita katika Mahafali ya 19 ya Shule ya Wasichana ya St. Marys Mazinde Juu wakiwa katika mahafrali hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali wakati wa kuwasili katika eneo la Mahafali ya 19 ya kidato cha Sita ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Lushoto Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana Mku wa shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Sister Evetha Kilamba wakati wa kuwasili katika eneo la Mahafali ya 19 ya kidato cha Sita ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Lushoto Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwapungia mkono wanafunzi wa kidato cha sita wakati wa mahafali ya 19 ya shule ya Wasichana ya St. Mary's Mazinde Juu. Wakati wa kuwasili ukumbi wa hafla hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika tukio hilo la mahafali ya 19 ya kidato cha sita shule ya St. Mary's Mazinde Juu,
Wanafunzi hao wa kidato cha Sita wakiwa katika tukio hilo

Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Ndugu Elishilia Kaaya akitoa maelezo machache namna wanavyoendesha shule hiyo pamoja na kuwahusia wanafunzi hao wanaohitimu 
Mwenyekiti wa Bodi, Ndugu Elishilia Kaaya akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla
Umati mkubwa wa wazazi, walimu na wanafunzi pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo

No comments: