ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 9, 2016

MAPITIO YA HOJA MBALIMBALI ZA WABUNGE MJINI DODOMA

Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani akijibu baadhi ya hoja za Wabunge zilizoihusu Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kipindi cha jioni Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) (kulia) akijibu baadhi ya hoja za baadhi ya Wabunge wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali jioni bungeni mjini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa mapitio ya baadhi ya hoja za Wabunge leo jioni Bungeni mjini Dodoma. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mhe. Amina Makilagi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali za Wabunge leo mjini Dodoma. 
Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali Bungeni mjini Dodoma. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) akijibu hoja za Wabunge mbalimbali wakiochangia hotuba ya Wizara yake leo jioni Bungeni mjini Dodoma. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa mapitio ya hoja za Wabunge jioni Bungeni mjini Dodoma. 

(Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma)

No comments: