Tarehe 29 Aprili, 2016 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya heshima jijini Toronto, Canada. Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Konseli wa Heshima, Bw. Deepak Ruparell na Mhe. Jack Mugendi Zoka Balozi wa Tanzania Nchini Canada ambaye aliiwakilisaha Serikali ya Tanzania. Tukio hilo lilifanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Ottawa nchini Canada.
Fuatilia matukio katika picha.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada akimkaribisha Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell kwenye chumba cha wageni cha Ubalozi mara baada ya kuwasili.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Konseli wa Heshima Mteule,
Bw. Deepak Ruparell (kushoto) na Bw. Adtya Jha (kulia), Mjumbe wa National Capital Commission, Ottawa
ambaye alifuatana na Konseli wa Heshima Mteule.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada (mwenye tai ya Bendera ya Taifa)
akiwa katika picha ya pamoja na Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell (kulia kwa Balozi),
akfuatiwa na Bw. Richard Masalu, Afisa
wa Ubalozi na mwisho kushoto ni Bw. Leonce Bilauri, Mkuu wa Utawala Ubalozini.
Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bibi Aziza Bukuku
akifuatiwa na Bw, Paul Makelele ambao ni maafisa wa Ubalozi.
Tukio la kutiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya
heshima jijini Toronto, Canada likifanyika kati ya Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Nchini Canada ambaye anaiwakilisha
Serikali ya Tanzania na Konseli
wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell , likishuhudiwa na maafisa wa Ubalozi.
Baada ya tukio la kutiliana saini mkataba, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka na
Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell ,
wanaonekana wakibadilishana nyaraka za tukio hilo.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada anaonekana akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini
Toronto, Bw. Deepak Ruparell picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kwa
ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw.
Deepak Ruparell picha ya Baba wa Taifa, Mwl, Julius Kambarage Nyerere kwa ajili
ya matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada akimpa maelezo Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto,
Bw. Deepak Ruparell na hatimaye
kumkabidhi Nembo na Bendera ya Taifa kwa
ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada akimkabidhi Konseli wa
Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell nakala ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1963
kuhusu Utendaji wa Shughuli za Kidiplomasia na Taratibu za Kikonseli ikiwa ni moja ya vitendea kazi muhimu kwa
matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Canada (mwenye tai ya Bendera ya Taifa)
akiwa katika picha ya pamoja na Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini
Toronto, Bw. Deepak Ruparell (kulia kwa
Balozi) pamoja na wafanyakazi wote wa Ubalozi mara baada ya kuhitimisha tukio
la kutiliamna saini mkataba.
No comments:
Post a Comment