Mkazi mmoja mkoani Mwanza, Mshambuzia Bishanga amefariki dunia wakati akijaribu kuopoa simu yake ya mkononi iliyokuwa imezama Ziwa Victoria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea Juni 15 saa 6.38 mchana eneo la Mwaloni, Kata ya Kirumba wilayani Ilemela baada ya simu yake kudondokea majini.
“Baada ya kudondosha simu, akiwa hapo mwaloni aliamua kuingia majini kuitafuta, lakini maji yalimzidi nguvu na kushindwa kujiokoa,” alisema Msangi.
No comments:
Post a Comment