Friday, June 3, 2016

ASKOFU DK. ABEDNEGO NKAMUHABWA KESHOMSHAHARA AZURU MIJI YA NEW YORK, CHICAGO & MINNEAPOLIS, MAREKANI

Askofu Dk. Abednego Keshomshahara, Bibi Melisa Keshomshahara na Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mchungaji Elmereck Kigembe watembelea Marekani mwezi Mei 2016. Mei 15 hadi 21 walikuwa New York ambapo walihudhuria mkutano mkuu wa Synod ya Metropolitan New York ya Kanisa la Kiinjili Kilutheri Marekani inayoongozwa na Askofu Robert Alan Limbo. Mei 22 - 30 walikuwa Chicago na walipata fursa ya kukutana na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Marekani akiwemo Mkuu wa Kanisa hilo Askofu Elizabeth Eaton. Mwisho kabla ya kuondoka walifika Minneapolis, Minnesota walipokutana na Watanzania & marafiki wa Tanzania. Kwa ujumla ziara yao ilikuwa na mafanikio makubwa muno.

No comments: