Advertisements

Friday, June 17, 2016

DAWA ZA MILIONI 294 ZILIZOKAMATWA KATIKA OPERESHENI ZAKABIDHIWA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea dawa kutoka kwa Msajili wa baraza la Famansia , Elizabeth Shakalaghe ambazo walizikamata katika operesheni safisha maduka ya dawa   leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymont Mushi akipokea baadhi ya maboksi ya dawa jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BARAZA la  Famasia Tanzania  limekabidhi dawa  kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda zenye thamani ya Sh. milioni 294 zilizokamatwa katika operesheni safisha maduka ya dawa  iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi dawa  hizo Msajili wa baraza hilo, Elizabeth Shakalaghe amesema operesheni hiyo iliyofanyika katika Mikoa tisa na walifanikiwa kukamata dawa  zenye thamani ya zaidi ya  Sh. milioni 336 na kati ya dawa  hizo dawa  zenye thamani ya zaidi ya  Sh milioni 11 hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Alisema dawa hizo zitasambazwa katika hospitali zote za mkoa wa Dar es Salaam na zimehakikiwa.

Amesema katika Mkoa wa Dar es Salaam majalada 10 yamefunguliwa  mahakamani kwa wale waliokamatwa  na dawa  za serikali ambayo kwa sasa yapo katika hatua za upelelezi. 

"Bado kumekuwa na ongezeko  la maduka ya dawa ambayo yanaanzishwa kinyume na sheria na taratibu hususani katika Mkoa huu na tumebaini kwamba maduka yaliyofugwa wakati wa operesheni yanafunguliwa wakati wa usiku na kuendelea kutoa huduma za dawa .amesema.

Elizabeth amesema lengo la operesheni hiyo lilikuwa ni kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kuvunja sheria ya famasi katika uendeshaji na utoaji wa huduma za dawa nchini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa dawa hizo, Mkuu wa Mkoa huu,Paul Makonda alisema wamiliki wa maduka ya dawa ambao hawana vibali wanatakiwa kufunga maduka hayo mara moja au kuzirudisha walikonunua  huku wengine wakifanya huduma nyingine ambayo ni tofauti na leseni walizoomba.

Makonda amevitaka  vyombo vya dola na watendaji wa ngazi ya mkoa , manispaa, kata na mitaa kuhakikisha wanayafunga na kuyaondoa maduka yote ambayo hayana vibali na yanayoendeshwa kinyume na sheria ya famansi nchini.

Aidha amevitaka vyombo vya dola kufanya operesheni nyakati za usiku ili kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki kwa wale watakaokaidi maagizo ya awali na kufanya biashara wakati wa usiku kwa kizingizio serikali imelala wakati huo.

1 comment:

Machiri said...

inshallah maneno makubwa