Advertisements

Thursday, June 23, 2016

DAWATI KWA KILA MTOTO (A Desk For Every Child)

 Siku ya leo kwa mara nyingine tuko mkoa wa Mtwara, kukabidhi Reading Corners ama kona za kusomea katika shule mbili, Lilungu na Nanguruwe. Jumla ya vitu tulivyokabidhi ni madawati 60, makabati ya vitabu 4, vitabu 181, chati za mfano, herufi, hisabati pamoja na vifaa vya sanaa kama rangi za kuchorea, na kadhalika.
Mchango huu ni sehemu ya mradi wa DAWATI KWA KILA MTOTO (A Desk For Every Child) ambao umedhaminiwa na Shirika la marekani 'We are the world kids kama sehemu ya mpango wao wa kimataifa kujenga na kuanzisha maktaba na kona za kusomea kwa ajili ya shule za msingi na sekondari katika afrika na mashariki mwa Asia.'
 Mgeni wa heshima katika sherehe hii ni Mh. Halima Dendego -Mkuu wa Mkoa Mtwara, akiongozana na Mh.Fatuma Ally - Mkuu wa Wilaya Mtwara.
Sherehe hii ilifanyika katika shule ya msingi Lilungu (Mikindani).

1 comment:

Anonymous said...

Congratulations Hassan Maajar Trust for your effort to improve the learning environment in our primary schools. Big up