Advertisements

Friday, June 24, 2016

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA HUENDA IKASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UTENGENEZAJI MADAWATI

Na EmanuelMadafa,Jamiimojablog

Halimashauri ya jiji la Mbeya huenda ikashindwa kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuri, lililozitaka halmashauri kuhakikisha zinamaliza tatizo la uhaba wa madawati shuleni ifikapo Juni 31, mwaka huu kutokanana kutokuwepo kwa msukumo wa kutosha katika utekelezaji wa agizo hilo.

Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imeweza kutengeneza na kukamilisha madawati 1500, wakati uhitaji ni madawati 10,000.

Katika upungufu huo, shule za msingi zinauhitaji wa madawati 9894, wakati sekondari zikihitaji madawati 605.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa utengenezaji wa madawati katika chuo cha ufundi VETA jijini Mbeya , Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Mussa Mapunda, alisema katika madawati hayo 1500 ambayo tayari yamekamilika, madawati 798 ni ya shule za msingi huku madawati 477.

Alisema, kupatikana kwa madawati hayo 477 kwa shule za sekondari halmashauri itakuwa imemaliza deni kwa upande huo na kubaki na deni la madwati 9096 kwa shule za msingi ambao nayo yapo katika mchakato wa kukamilika.

Akizungumza na baadhi ya wananchi wakiwemo wanafunzi, madiwani na watumishi wa serikali, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi, alisema madawati 9096 ambayo yanahitajika katika shule za msingi yapo katika mchakato wa kukamilika.

Aidha, Meya huyo alisema, licha ya halmashauri hiyo kukabiliwa na changamoto ya rasilimali fedha lakini imeweza kufanya kazi hiyo kwa haraka hasa ukiangali ni kipindi kifupi tu, tangu kuungua moto kwa mabweni zaidi ya mawili ya shule ya sekondari ya iyunga na kuteketeza vitanda 150 na magodoro yake.

“Ninawashukuru wadau kwa kujitolea kwani wakati wakichangia shule ya Iyunga, suala la madawati nalo likaingia hivyo ninaamini kwamba halmashauri itaweza kukamilisha tatizo la madawati na wanafunzi wote kuondokana na tatizo la kukaa chini,”alisema.

Mwisho.

1 comment:

Anonymous said...

June ina siku 30 tu, kwa hiyo tarehe ilyotajwa (June 31) siyo sahihi