ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 28, 2016

JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI WAKATI WA MECHI YA YANGA NA TP MAZEMBE JIJINI DAR ES SALAAM LEO



RPC Ilala Salum R. Hamduni

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mchezo huo wenye mvuto mkubwa kwa washabiki wa Tanzania, nchi za Afrika mashariki na Afrika nzima kuchezwa katika hali ya usalama.
Aidha tunaomba wananchi wasiwe na shaka yoyote ya kiusalama na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa nje au ndani ya uwanja. 
Kutakuwa na CCTV Camera ili kuhakikisha sehemu zote mageti ya kuingilia na kutokea na maeneo yote yanaonekana na kuweka kumbukumbu za matukio yote.
Pamoja na hayo wananchi wanatakiwa kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:

·        Kuingia na chupa za kimiminika cha aina yeyote,
·        Kuingia na silaha ya aina yoyote
·        Kupaki magari ndani ya uwanja
·        Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziwaruhusu.
  
SALUM. R. HAMDUNI
KAMANDA WA  POLISI MKOA IALA


DAR ES SALAAM

No comments: