Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto),
akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuwasili katika kituo
cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya
Mombasa-Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua
na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius Magoma, akimuelekeza jambo Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya
ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji
wa raia wa kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga, jijini
Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, DCI Andrew Kalengo, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, mara baada ya
kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa
kiraia), akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya Uhamiaji Wilayani Nkinga, mara baada ya
kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini
kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la
kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto),
akionyeshwa namba za jiwe la mpaka unaotenganisha nchi za Kenya na Tanzania mara baada ya
kutembelea kituo cha Uhamiaji Horohoro. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi
ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment