ANGALIA LIVE NEWS
Sunday, June 5, 2016
Majambazi 3 Wauawa Katika Majibizano ya Risasi na Polisi Mwanza
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI LEO TAREHE 05.06.2016
KWAMBA MNAMO TAREHE 03.05.2016 SIKU YA IJUMAA ASKARI POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WALIFANIKIWA KUMAKAMATA OMARY FRANCISKITALETI@KIBERITI, MUUNGULIMI MIAKA 28 MFANYABIASHARA WA BUCHA YA NYAMA YA NG’OMBE NA MKAZI WA NYEGEZI- KIJIWENI BAADA YA KUPEWA TAARIFA NA RAIA WEMA YA MTU HUYO KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWENYE MADUKA YA M-PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY JIJINI HAPA, NA ALIPOHOJIWA NA ASKARI POLISI ALIKIRI KUHUSIKA KATIKA MATUKIO HAYO NA ALIWATAJA WENZAKE WANAOSHIRIKIANA NAO NA MAHALI WALIPOJIFICHA.
Omary Francis Kitaleti @Kiberiti, mmoja wa majambazi aliyeuawa na wenzake kwa risasi.
AIDHA TAREHE 04.06.2016 MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU ALIKUBALI KWENDA KUWAONYESHA ASKARI POLISI MAFICHO YA WENZAKE YALIYOKUWEPO KWENYE MAPANGO YA MLIMA WA UTEMINI KATA YA MKOLANI WILAYANI NYAMAGANA, MAJIRA YA SAA 17:00HRSPOLISI WALIFIKA KATIKA MLIMA HUO NA WALIPOYAKARIBIA MAPANGO HAYO GHAFLA WALIANZA KUSHAMBULIWA KWA RISASI NA MAJAMBAZI WALIOKUWA WAMEJIFICHA NDANI YA MAPANGO HAYO. KATIKA MAPAMBANO HAYO YA RISASI NA ASKARI POLISI, RISASI HIZO ZILIWEZA KUMPATA JAMBAZI MWENZAO AITWAYE OMARY FRANCIS KITALETI @ KIBERITIALIYEKUWA ANAWAONGOZA ASKARI POLISI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO, NA RISASI NYINGINE ILIMJERUHI ASKARI KWENYE UNYAYO WA MGUU WA KULIA.
KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI NA MAJAMBAZI HAYO KWENYE MAPANGO YA MLIMA WA UTEMINI, ASKARI POLISI WALIFANIKIWA KUMUUA JAMBAZI MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 20 HADI 25 AMBAYE ALIKUA AKIWASHAMBULIA POLISI KWA KUTUMIA BASTOLA. BAADA YA POLISI KUMPIGA RISASI JAMBAZI HUYO WALIMPEKUA NA KUMKUTA AKIWA NA BASTOLA AINA YA CHINESE YENYE NAMBA M.20-06436 ILIYOKUWA NA RISASI TATU NDANI YA MAGAZINE, WAKATI HUO MAJAMBAZI WENGINE WALIOKUWEPO KWENYE MAPANGO HAYO WALIENDELEA KUJIBISHANA KWA RISASI NA ASKARI POLISI.
POLISI KWA KUTUMIA MBINU ZA MEDANI ZA KIVITA WALIWEZA KUZINGIRA MAENEO HAYO YA MLIMA WA UTEMIA HADI ALFAJIRI YA KUAMKIA LEO HUKU WAKIJIBISHANA RISASI NA MAJAMBAZI HAO, BAADA YA MAJAMBAZI HAO KUONA WAMEZIDIWA NGUVU NA KUMEKARIBIA KUPAMBAZUKA NDIPO WALIAMUA KUONDOKA NDANI YA MAPANGO HAYO KWA KURUSHA BOMU MOJA LA KUTUPA KWA MKONO HUKU WAKIZIDISHA MAPIGO YA RISASI KWA KUTUMIA SILAHA WALIZOKUWANAZO.
PAMOJA NA MAJAMBAZI HAO KUFANIKIWA KUTOROKA KATIKA MAPANGO HAYO, WANANCHI WALIWAONA ASUBUHI NA WAKAWATILIA MASHAKA NDIPO WALIWAJULISHA POLISI KUWA KUNA WATU WATATU WAMETOKA KWENYE MAPANGO HAYO NA KUKODI PIKIPIKI HUKU WENGINE WAKIKODI TAXI WAKIELEKEA MTAA WA NYASAKA. TAARIFA HIZO ZILIWASAIDIA ASKARI POLISI KWANI WALIFANIKIWA KUWAFUATILIA MAJAMBAZI HAO HADI MAENEO YA MTAA WA NYASAKA AMBAPO WALIFANIKIWA KUMUONA JAMBAZI MMOJA NA BAADA YA JAMBAZI HUYO KUBAINI KUWA ASKARI POLISI WALIKUA WANAMFUATILIA ALITOA BUNDUKI NA KUTAKA KUWAPIGA ASKARI POLISI NDIPO POLISI WALIMUWAHI NA KUMFYATULIA RISASI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.
JAMBAZI HUYO ALIYEUAWA ALITAMBULIWA KWA JINA LA SAIDI KHAMISI MBULI @ FUNDIBOMBA MNYATURU MIAKA 48 MKAZI WA BUGARIKA , BAADA YA KUMUA JAMBAZI HUYO POLISI WALIFANIKIWA KUPATA BUNDUKI MOJA AINA YA SMG YENYE NAMBA 307039ILIYOKUWA NA RISASI NANE NA KISU KIMOJA, HUKU WENZAKE WAWILI WALIFANIKIWA KUTOROKA LAKINI BADO ASKARI POLISI WANAWAFUATILIA NA MSAKO MAKALI UNAENDELEA.
PIA ASKARI POLISI WALIWEZA KUFANYA UPEKUZI KWENYE MAPANGO YA MLIMA WA UTEMINI NA KUFANIKIWA KUPATA VITU TOFAUTITOFAUTI VILIVYOACHWA NA MAJAMBAZI HAO AMBAVYO RISASI NNE, KISU KIMOJA CHENYE DAMU, KOFIA YA KUFICHA USO NYEUSI MOJA (MASK), JIKO LA STOVA, MASUFURIA YA KUPIKIA, UNGA WA MAHINDI,SUKARI, DAGAA, CHAKULA KILICHOPIKWA ,NGOMA MBALIMBALI, NA SIMU TATU ZA MKONONI. ASKARI ALIYEJERUHIWA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI, POLISI BADO WANAENDELEA NA MSAKO WA KUWATAFUTA MAJAMBAZI WALIOFANIKIWA KUTOROKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI, ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA WATULIE NA WATOE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI TUWEZE KUHAKIKISHA UHALIFU TUNAUTOKOMEZA KATIKA MKOA WETU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Tanzania tu wagumu kujifunza.Miaka ya nyuma,kulitokea mapambano kati ya majambazi na polisi kwenye mapango hayox2.Tukio la majambazi kurudi na kuweka kambi katika mapango hayo ni kielelezo kuwa polisi wetu wana deal na tukio kama linavyojitokeza,likiisha basi.Amboni,Tanga the same story...
Post a Comment