Advertisements

Wednesday, June 22, 2016

Mtoto abakwa na kunyongwa jijini Arusha

Eneo la Unga Limited, jijini Arusha

Mtoto wa miaka minne amebakwa na kuuawa kwa kuvunjwa shingo na kutupwa kandokando ya njia ya watembea kwa miguu karibu na mfereji wa maji umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuf Ilembo amesema tukio la kubakwa kwa mtoto huyo wa kike lilitokea Machi 20 mwaka huu saa 3:3O usiku kwenye makaburi ya Baniani kata ya Ungalimited .
Ilembo amedai mtoto huyo ambaye kwasasa ni marehemu alikuwa akicheza na wenzake nje kidogo ya nyumbani kwao na ilipofika majira ya saa 12:00 jioni kwa mujibu wa marafiki zake (majina yamehifadhiwa) wanasema alifika mtu mmoja mwanaume mrefu akiwa amevaa suruali na kumwambia marehemu amfuate akamnunulie pipi na hapo ndipo marehemu alipomfuata huyo na hakurudi tena.

Amesema ilipofika majira ya saa 1:30 usiku baada ya wazazi kuona mtoto wao amechelewa kurudi nyumbani ambapo si kawaida yake kuchelewa walianza kumtafuta kwa kuwataarifu majirani pamoja na kutoa taarifa katika msikiti wa Esso.

Amesema baadaye kidogo wakapokea taarifa za mtoto kuonekana katika njia ya watembea kwa miguu katika makaburi ya baniani akiwa amekufa ndipo walipotoa taarifa kituo kikuu cha Polisi Wilaya ya Arusha Mjini.

Kisha polisi waliuchukua mwili wa mtoto huyo na kuupeleka Hospitali ya Mount Meru kwaajili ya uchunguzi zaidi na baada ya uchunguzi imebainika kuwa marehemu alibakwa na kuvunjwa shingo kitendo kilichosababisha kifo chake.

Hata hivyo kutokana na tukio hilo polisi inawashikilia watu watano kuhusiana na tukio hilo na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria na marehemu huyo jina tunalo amezikwa katika makaburi ya Kwamrombo.

Polisi inatoa wito kwa wanaume wenye tamaa chafu au wanaotumia imani za kishirikina kuacha mara moja tabia hizo chafu za kuwanyanyasa watoto wa kike na kusababisha mauaji kama hayo.

No comments: