ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 17, 2016

NDEGE YA PRECISION AIR YANUSURIKA KUWAKA MOTO ZANZIBAR

Ndege ya Precision Air ikitokea Kilimanjaro kuelekea Dar es salam kupitia Zanzibar usiku wa Alhamisi ili pata hitilafu ya injini yake moja kushika moto wakati ikitaka kuruka Uwanja wa Kimataifa wa Karume wa Zanzibar na kupelekea abiria  kushuka haraka na kurejea sehemu ya mapokezi. Hakuna madhara ambayo yameripotiwa na abiria wote walishuka salama,
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, mojawapo ya injini ilishika moto  na kulazimisha marubani  kusimamisha ndege na kuirudisha sehemu ya kupakia abiria, baada ya kuchukua hatua za dharura za kuuzima moto huo kabla ya kuleta madhara.  
Kampuni ya Precision imethibitisha tukio  hilo na hii hapa tarifa yake rasmi