Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amewaapisha wakuu wapya wa wilaya 139 na wakuu wa mikoa wanne kwenye hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akiwa na baadhi ya wakuu wa wilaya kwenye picha ya pamoja Ikulu Jumatano hii
Miongoni mwa wakuu wa wilaya wapya ni mtangazaji nguli wa redio na TV, Godwin Gondwe. Gongwe sasa ni mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Akiongea kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli anayefahamika kwa utani mwingine alimsifia Gondwe kuwa ni mtangazaji mzuri na kumtaka atumie uwezo huo kutangaza maendeleo.
“Gondwe najua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu,” alisema.
Godwin Gondwe kama anavyojulikana pia alikuwa mtangazaji maarufu wa habari kwenye kituo cha runinga cha ITV. Amewahi pia kufanya kazi kwenye vituo vya redio vya Radio Free Africa na Radio One. Lakini pia alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment