Tuesday, June 7, 2016

Upepo wa Lowassa wazidi kuyumbisha CCM

By Joyce Joliga na Tausi Mbowe, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dodoma/Songea. Wabunge wa CCM wameunda kamati maalumu ya wabunge 15 kwenda kutathmini uchaguzi mkuu, badala ya kutegemea ripoti zinazotolewa na makatibu wa wilaya na mikoa pekee.

Katibu wa wabunge hao, Jason Rweikiza alisema kamati ya wabunge hao itawahoji wabunge wote wa CCM 267 kwa sababu ndiyo wahusika wakuu, kuangalia changamoto walizokutana nazo.

Miongoni mwa wajumbe hao ni Joseph Mhagama, Dk Faustine Ndugulile, Joseph Kakunda, Profesa Anna Tibaijuka, Mboni Mhita, Peter Serukamba, Innocent Bashugwa, George Mkuchika, Munira Mustapha, Jasmini Tiisekwa na Abdallah Ulega.

Katika hatua nyingine, CCM Mkoa wa Ruvuma imewatimua wanachama 62 kwa usaliti ikiwamo kumuunga mkono Edward Lowassa katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitiawww.epaper.mcl.co.tz

1 comment:

Anonymous said...

Huo si upeo wa EL bali hizo ni siasa tu Afrika. Huyo huyo EL alikimbia sisiemu kuogopa kuwa jipu tambaazi, Ukawa nao wakakutana na hayo hayo ya EL hata kumpa nafasi ya kuombea urais. Kwa kifupi EL hana upeo wa kulitesa li sisiemu ila yeye anateseka kwa kukubali kuwa jibu.