Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.
3 comments:
Hmmmm!
Hivi tukisema wabunge wa upizani ni watu wasiokuwa makini wala wasiojitambua na wapuuzi hadi unajiuliza kama na hao wananchi walipowapeleka pale bungeni ni wapuuzi au tena ni hiyo habari ya rushwa iliotawala katika jamii yetu ya kitanzania ndicho chanzo cha upinzani kupatikana kwa wabunge wa hovyo. Huyo mbilinyi nasikia aliishi hapa marekani,kama kweli aliishi Marekani siwezi kutajia kwa mtu wa nafasi kama yake kufanya kitendo alicho kiri kufanya,yaani ni umbavu wa hali ya juu. Ndugu mbilinyi anaelewa kabisa kwa mtu mwenye nafasi kama yake na kitendo alichokifanya isiwe ndani ya bunge iwe mitaani huko na kiripotiwe na vyombo vya habari kwa marekani basi political career ya mtu kama huyo is absolutely over. Nashangaa hata mwenyewe anashindwa kuchukua nafasi ya kujihukumu mwenyewe kwa kujiuzulu kwa hakika adhabu aliopewa ni ndogo mno kulingana na kosa alilotenda. Yaani mbunge mwakilishi wa wananchi anakwenda kunyanyua kidole cha kati(the middle finger) ndani ya bunge alafu bado anatembea kifua mbele, yaani inasikitisha .Sasa kama mtarajiwa wa kuwa mfano katika jamii anayoiongoza kwa kitendo alichokifanya atakuwa anafundisha nini. Labda wasioelewa maana halisi ya mtu kunyanyulia kidole cha kati kwa staili alioionyesha ndugu Mbilinyi ni kumwambia mtu kuwa Anafi..r..warai kwa tamaduni yetu ya kitanzania sifikirii tunahitaji viongozi wa aina hii.
Hawa watu sio viongozi wameenda Bungeni kufanya vituko na fujo tu kuanzia Hao viongozi wao wanaojiita UKAWA, hawajakomaa kabisa hata Kisiasa, kwa maoni yangu naona hata serikali Inawalea wanatakiwa washikishwe adabu!
Post a Comment