Advertisements

Friday, June 24, 2016

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.

Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.

Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.

Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.

BBC

1 comment:

Anonymous said...

Ni vyema kama nchi zilizotawaliwa na Uingereza nazo zijitoe katika Commonwealth. Viongozi wa nchi za kiafrika kwenye commonwealth jaribuni kutafakari hali hii ili nanyi mjiodoe na umoja huo. kama Waingereza hawataki kuwa wamoja na wenzao Ulaya, basi kwa nini mataifa ya Commonwealth yawe na umoja na Waingereza?