Advertisements

Friday, June 24, 2016

WAZIRI MWIGULU AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA POLISI NA UHAMIAJI CCP, MJINI MOSHI LEO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkabidhi zawadi mhitimu Irene Joji (kushoto) kwa kufanya vizuri katika masomo yake wakati wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba mjini humo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikagua gadi ya wahitimu wa Jeshi la Polisi na Uhamiaji kabla ya kuyafunga mafunzo ya wahitimu hao wa mafunzo ya awali yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikagua gadi ya wahitimu wa Jeshi la Polisi na Uhamiaji kabla ya kuyafunga mafunzo ya wahitimu hao wa mafunzo ya awali yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo leo

Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji wakimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) jinsi miili yao ilivyokuwa imara kwa pikipiki kupita juu ya matumbo yao. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba mjini humo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini Moshi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji, kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments: