Klabu ya Yanga imeamua kutoa fursa kwa mashabi wake na mashabiki wa soka la Tanzania kuingia bure kwenye mchezo wao wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe miamba ya soka la DR Congo mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumanne June 28 kwenye uwanja wa taifa.
Taarifa iliyotolewa na afisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Cornel Muro inazomeka hivi: “Mechi ya Yanga na TP Mazembe Jumanne 28-06-2016, mashabiki wote wanaruhusiwa kuingia uwanjani BURE bila ya kiingilio, lengo likiwa ni kuwahakikishia WATANZANIA wanapata nafasi ya kui-support timu yao ya Yanga.”
No comments:
Post a Comment