Advertisements

Tuesday, June 28, 2016

ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA LAANZA KWA VYAMA VILIVYOPO DAR ES SALAAM

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kulia) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa NLD Tozzy Ephraim Matwanga.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe Bw. Ibrahim Mkwawa ( hayupo pichani) wakati wa uhakiki wa utekelezaji masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo jinini Dar es Salaam.

Bw. Ibrahim Mkwawa, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe “Monitoring” (katikati) akikagua nyaraka mbalimbali za Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhasibu Bi. Severa Assey kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Bw.Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini akihoji taarifa za fedha wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa chama cha NLD Jijini Dar es Salaam leo . Katikati ni Mwenyekiti wa chama , Bw. Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Tozzy Ephraim Matwanga ( kulia )
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa uperembe Ibrahim Mkwawa (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam leo. Picha na MAELEZO

No comments: