ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 28, 2016

PICHA: MASHABIKI WA YANGA WAFIKA UWANJANI ALFAJIRI WAKISUBIRI KUINGIA UWANJA WA TAIFA

Klabu ya Yanga leo June 28 inaingia uwanjani katika mechi ya kombe la Shirikisho inawaalika klabu ya TP Mazembe kutoka DR Congo mchezo ambao utachezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Mechi hiyo ambayo haina kiingilio ni bure tu kuingia uwanjani leo asubuhi mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Young Africans tayari wamejitokeza kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wakisubiri muda wa kufunguliwa milango.

Mashabiki hao wapo tangu alfajiri wakisubiri kupewa utaratibu wa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo.


1 comment:

Anonymous said...

Utaona hapa kiasi gani watanzania tunavyopenda vya bure yaani inahitajika elimu maalum ya kuelimishwa yakwamba kutumia pesa yako ulioifanyia kazi kwa kitu unacho kipenda ni raha zaidi kuliko kupata kitu kwa njia ya bure. Yaani kitendo cha kutangazwa kuwa kiingilio kitakuwa bure uwanja wa taifa ni kama dream come true kwenye vichwa vya watanzania wengi hasa vijana yakwanba labda ipo siku ataibua zari la mtu kuja kumgaia pesa bure labda kaka au mjomba au kumkwaa mwanamke mwenye hela,au hata ndoto ya kuokota hela nyingi na ndoto hizo kama hazija jibu na mara nyingi ndivyo inavyotokea basi utaona kijana analazimisha kwa kujiingiza katika vitendo vya kihalifu kama utapeli,wizi wa kutumia nguvu nakadhalika nakadhalika. Inanikumbusha Uswisi japo tunatofautiana kimambo mengi hasa kiuchumi yakwamba wenzetu wametoka zamani na ni miongini mwa nchi chache duniani zenye utajiri wakutisha lakini utajiri wao hawakuupata kwa kukaa tu na kuota bali walifanya kazi kinguvu na zaidi akili. Ikumbukwe unapoteseka katika kutafuta kitu chochote basi kama utakaa chini na kuipa mazoezi akili nao ifikiri nini cha kufanya ili mafanikio yapatikane basi na akili nao inakuwa zaidi yaani akili inahitaji mazoezi katika jambo fulani na kama mtu atakaa tu basi na akili nao inakaa. Uswisi ilipigwa kura ya maoni kuwaliza wananchi wake kama wapo tayari kupewa pesa za bure kila mwezi yaani pesa za kumkizi mtu matumizi yake yote kwa mwezi mzima na haijalisi kama uanafanya kazi au la Serikali ya uswis inataka kuwapa wananchi wake pesa za bure kila mwezi kwa hivyo wakauliza wananchi wake kwa kura ya maoni lakini matokeo ya kura yakaja yakwamba wananchi wamekataa kupewa pesa za bure wamesema kufanya kazi na kutumia ulicholipwa baada ya kufanya kazi ni bora zaidi. Waswisi hawawezi kuamua kukataa pesa za bure kama si tabia nzuri iliojengeka katika jamii yao kwa muda mrefu ya kufanya kazi na kuishi kutokana na kile ulichokifanyia kazi na si vingine. Waswahili wanasema takrima ikizidi ni hatari zaidi kwa mwenye kukirimiwa.