Advertisements

Sunday, July 10, 2016

ABIRIA WAKWAMA UBUNGO KWA KUKOSA MABASI



Picha na Mpigapicha wetu.
By Ephrahim Bahemu, Mwananachi ebahemu@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. ongezeko la abiria hasa wanafunzi limesababisha upungufu wa mabasi yanayotoa huduma kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani na kusababisha wasafiri wengi kukwama.

Abiria hao wameonekana wameketi chini kusubiri usafiri bila matumaini na wengine wakiwa katika foleni ndefu kwa ajili ya kukata tiketi ili kujihakikishia safari kesho.

Mmoja wa wakatisha tiketi, Shaffik Ally amesema tatizo la usafiri lipo zaidi kwa mabasi ya Morogoro, Moshi, Arusha na Iringa.

“Kwa mikoa ya mbali kama Mwanza, Mbeya, Kagera na Kahama ukitaka tiketi siku mbili kabla ya safari hakuna shida na unapata usafiri wa uhakika, lakini mikoa hii ya karibu ambayo watu walizoea hata kuja asubuhi na kupata usafiri, hali imekuwa tofauti kabisa,” amesema.

Meneja Mawasiliano Sumatra, David Mziray amesema tatizo hilo ambalo limetokea tangu jana Jumamosi limesababishwa na wingi wa wanafunzi wanaorejea shuleni baada ya likizo.

Amesema mamlaka hiyo inachokanya sasa ni kuthibiti kusiwepo na ongezeko la nauli.

“Upungufu wa mbasi upo na huwezi kusema uongeze mabasi mapya leo, haiwezekani.

Amesema mamlaka imechukua hatua ya kuhamasisha wamiliki wa mabasi ambayo safari zake hazina abiria wengi kuleta mabasi kwenye safari hizi zenye mahitaji makubwa na tayari wameitikia wito na mamlaka imeanza kutoa vibari vya muda kwa magari hayo,” amesema Mziray.

No comments: