Advertisements

Monday, July 4, 2016

BALOZI WILSON MASILINGI KUFANYA ZIARA SEATTLE, JIMBO LA WASHINGTON

Ndugu Watanzania wenzangu,

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani HE.Wilson M. Masilingi atafanya ziara kwenye jimbo letu la Washington State. Atatembelea Kiwanda cha ndege za: Boeing - Everett, Kampuni ya Starbucks - Seattle na kukutana na umoja wa wafanyabiashara wa Seattle (Seattle Chamber of Commerce) na pia atafanya mazungumzo na watanzania wa eneo letu..

Mkutano na watanzania utafanyika kama ifuatavyo:

Siku: Jumamosi Tarehe 16, Julai, 2016
Saa: 10 jioni hadi saa 1 jioni. (4PM -7PM)

411 156th Ave Ne
Bellevue, Wa 98007

''Landmark = Near Crossroads Mall, Bellevue''

Tafadhali saidia kusambaza ujumbe huu na kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa Habari Bw. Abdul Dola 206 422 3050.

Munaombwa kuhudhuria kwa wingi.


Ahsanteni Sana.
Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Seattle.

Wenu,
Katibu - Haji Rajab Haji

No comments: